MWANAUME SIKIA HII ......


Image result for MAISHA YA UPENDO YA MUME & MKE YANAJIONYESHA KWA MAMBO YAFUATAYO
USIJE ukafikiria hata siku moja kwamba unamkomoa mwanamke kumzalisha na kumkimbia,hata siku moja humkomoi sana utampa maumivu ya mda ambayo baadae yatageuka kuwa chakula chenye nguvu ndani ya mwili.

Sawa atahangaika na mwanae,masika yote na kiangazi chote,atakula nae kile anachokula,atamvalisha nguo safi hata kama mtoto ana nguo tatu tu za kushindia.
Lakini mwisho wa siku utakuja kujigundua kwamba wewe ndio mpumbavu,kiumbe ulichomwachia ulidhani ni jiwe kwamba hakitakua na kupata maarifa.

Watoto kama hawa waliokataliwa sikufichi huwa wana akili na vipaji vikubwa sana.Wewe zunguka dunia,kaponde mali lakini kumbuka kwamba kuna uzee,hapo ndipo utakaporudi na kuanza kumtafuta mtoto wakati huo single mom anafurahia maisha na mwanae baada ya juhudi nzito za kumpigania afanikiwe.

Utakuja kugundua kwamba ulitupa jiwe ambalo ndani yake limeviringisha dhahabu,na ndipo mtoto nae anapokukataa.
Mungu azidi kuwabariki single Mom wote...Naimani ipo siku mtaivisha tu matunda yenu.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post