MWANAMKE NI KIUMBE ANAETAKIWA KUISHI KWA AKILI:


Kama kuna kiumbe anaetakiwa kuishi maisha yake kwa akili na maarifa ya kutosha basi ni mwanamke. Maisha ya mwanamke yameangaza kwenye kila kona ya dunia yan asipoishi kwa akili anaweza kupoteza muelekeo na hadhi ya maisha yake.
Naweza nikasema maisha ya mwanamke yapo uchi, ni maisha yanayoangaliwa na kila mtu, sasa kwakua maisha yako yapo uchi usipoangalia utachafuliwa na kuharibiwa kabisa. Maisha ya mwanamke yapo baina ya Kusifika na Kutumika.
Kila jambo linalofanya na mwanamke linaonekana kwa mapana zaidi, linaonekana kwa pande zote yan walioko mbele yake wanamuona, wanyuma yake wanamuona, wakushoto na wakulia hivyo hivyo. Sasa mwanamke ambaye hatambui yupo uchi katika pande zote za dunia atachafuliwa na kuharibiwa.
Mwanamke ni kioo kila mtu anajitazama kupitia wew awe mzuri, awe mbaya, awe mtoto awe mzee, lazima ajiangalie kupitia wew ambaye ni kioo. Kuna mambo ambayo yanafanywa nawanawake mpaka watu wanashindwa kumtizama yeye kama kioo.
Mwanamke amebeba sifa nyingi ambazo zinasababisha aonekane kama dira ya dunia, Atizwamwe na kila mtu. Mwananke anatizwamwa kama mama mlezi wa familia, mshauri mkuu kwa mabinti na vijana.
Mwanamke huyo huyo anatizwamwa kama Dada, msichana, binti mwenye kujiheshimu, kuyajua maisha yake, lakin pia mwanamke huyo huyo anatizwamwa kama kahaba, Malaya, kutokana na vilee ajiwemavyo.
Maisha yako yapo uchi lakin inategemea na mkao gani ambao umekaa kutokana na kwamba maisha yako yaoo utupu lakin yanaonekanaje. Vile ambavyo unafanya maisha yako yawe ndivyo yanavyoonekana kweny jamii na dunia nzima.
👉Unatakiwa uishi kwa akili maisha ya maarifa, ujuzi na ubunifu, Tambua dunia inakuangalia. Alafu ukishagundua upo uchi ebu fanya mambo ambayo hayata kudhalilisha, kukuchafua wala kukuharibu. Ishi maisha ya Kistaarabu maisha ya kuigwa na kila anaejitazama kupitia wew maana ww ni Kioo.
J4REAL


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post