🔴
TATIZO hili la mwanamke kukosa msisimko wa tendo la ndoa kitaalamu tunaita ‘Female Sexual arousal disorder’. Mwanamke akiwa na hali hii huwa hajihisi hamu wala haja ya kuhitaji tendo hilo na wakati mwingine huona kama usumbufu endapo atakuwa katika mahusiano.
🏃👇
Mwanamke wa aina hii kama yupo mwenyewe au ‘single’ haoni umuhimu wa kuwa na Mume au na hasa kama anajimudu kiuchumi. Wapo baadhi ya Wanawake wenye hali hii ambao hawana watoto au wengine wanamtoto mmoja au zaidi na aidha wameachana na Waume wao au Waume wao walishafariki.
👇
Msisimko hupatikana baada ya hamu ya tendo la kujamiiana kuwa juu ya kiwango na kusababisha mabadiliko mwilini na kusaidia mwili uwetayari kwa tendo. Hali ya msisimko kwa Mwanamke haina tofauti na hali ya Mwanaume kusimamisha uume wake. Mwanamke aliyepoteza msisimko huwa hajisikii chochote wakati wa ’ Romance’ au maandalizi ya tendo la ndoa, wengine huwa hawapati hamu na wengine hupata hamu kwa kiasi kidogo lakini hawapati mguso au msisimko.
👇
Tatizo la kutopata msisimko wa tendo la ndoa huambatana na dalili ambazo ni athari pia, endapo Mwanamke atapoteza msisimko wa tendo kwa muda mrefu basi mwishowe hawezi kufika kileleni na kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa. Mwanamke atagundua kama ana tatizo hili kwa kujihisi mkavu ukeni, uume unashindwa kupenya na hapati majimaji ya kulainisha uke katika kipindi chote anaposhiriki tendo hili.
👇
Vilevile atahisi ana uke mdogo kwani kila anapofanya tendo hili uume hauzami ndani na unaishia juujuu tu na hata kupenya ukeni inakuwa ngumu yaani kwa kawaida Mwanamke anapokuwa na msisimko wa tendo la ndoa, sehemu za uke na mashavu yake hujaa na kuwa na joto la kutosha, lakini Mwanamke ambaye hana hali hii uke wake unakuwa katika hali ya kawaida na mashavu au midomo ya uke inakuwa myembamba na mikavu yaani haijai ‘ Decreased genital tumescence or swelling.’
👇
Mwanamke aliyekosa msisimko huwa hajisikii chochote anapoguswa ukeni au kwenye chuchu zake au hujihisi kwa mbali sana‘ Decreased genital or nipple Sensations’. Hali ya msisimko wa tendo la ndoa pamoja na kuwa ni hali ya kisaikolojia, lakini kwa kiasi fulani husababishwa na matatizo ya kiutendaji kazi mwili ambayo kitaalamu inaitwa ’physiological’ huchangiwa na masuala ya vichocheo au homoni za kike endapo kutakuwa na mapungufu.
👇
Mtu yeyote, Mwanaume au Mwanamke, hali ya msisimko wa kimapenzi huchangiwa na hali iitwayo ‘Erotic Stimuli’ ambayo hutegemea na hali halisi mtu alipo au alivyo na msisimko huamshwa na mambo mawili tu ambayo ni hali ya kimwili na kiakili.
👇
Hakuna Mwanamke ambaye anatokea tu akakosa msisimko, tatizo la msisimko husababishwa na matatizo ya kisaikolojia zaidi ambayo huathiri hali ya utendaji kazi mwili endapo tatizo litakaa kwa muda mrefu. Matatizo kama msongo wa mawazo au ‘stress, ‘ Depression’ au sonona, akili kutokaa sawa kutokana na majukumu mazito, hasira za mara kwa mara, chuki dhidi ya mwenza au wanaume, matatizo au migogoro ya kimahusiano na kimapenzi, kutoku aminiana na Mume wako ni mojawapo ya vyanzo vinavyomfanya mwanamke akose msisimko wa tendo la ndoa.
🏃
Vyanzo vingine ni matatizo ya kimagonjwa au ‘medical factors’, kama tulivyoona hapo awali,mapungufu katika vichocheo au mfumo wa homoni mwilini, upungufu wa msukumo wa damu katika viungo vya ukeni, matatizo katika mfumo wa mishipa ya fahamu, pia matumizi ya baadhi ya madawa yawe ya hospitali au ya asili yanaweza kuathiri hali ya msisimko.
👇
Mwanamke mwingine anaweza kupatwa na tatizo hili baada ya kuolewa au hata kuachika mfano, alipokuwa na Mume wake wa zamani alikuwa anapata msisimko, lakini huyu wa sasa kila akijitahidi hapati msismko na wala hafurahii tendo la ndoa. Hali hii inaweza kuleta mgogoro endapo Mwanamke atajisahau na kumlinganisha wa zamani na huyu wa sasa. Mwanamke kukosa msisimko hutokana na kukosa hamu ya tendo la ndoa.
👇
UCHUNGUZI NA TIBA
👇
Katika tatizo hili uchunguzi huzingatia mambo mawili makuu, kwanza ni hali ya kisaikolojia‘ Psychological and emotional factors’ ambapo muhusika atapata tiba iitwayo ‘Sex therapy’ hasa kwa kuchunguza mahusiano, pili uchunguzi utazingatia hali ya mabadiliko kimwili ‘Medical factors’ ambayo hali ya uwepo wa magonjwa itaangaliwa au kuchunguzwa.
👇
Uchunguzi wa tatizohili huchukua muda mrefu. Katika uchunguzi wa kisaikolojia mambo matatu muhimu yataangaliwa kwa undani, kwanza niendapo mtu hana hamu au hapendelei kabisa hata kusikiliza habari zihusuzo masuala ya kimapenzi, ‘Abscent or Significantly reduced interest in Sexual activities’, pili nikutowaza au kufikiria lolote kuhusu msisimko au masuala ya kujamiiana ‘reduced interest in erotic thoughts of fantasies’. Mtu wa aina hii pia hushindwa kuanza kuongelea lolote kuhusu masuala ya mapenzi kwa kuhisi aibu au uwoga.
👇
Wakati mwingine hapati raha na hafurahii tendo la kujamiiana na uhisi kama anapoteza muda na kero kwake. Tiba ya tatizo hili ni dawa za homoni na kuongeza msukumo wa damu sehemu za siri pamoja na ushauri nasaha
Post a Comment