MOYO WA MWANAUME UNAHITAJI KUSHIBA SILAHA HIZI TATU:


👉LOVE 👉CARE 👉CONCERN
Sometimes Katika ndoa au mahusiano, ni muhimu moyo wa mwanaume uwe ni silaha za kuilinda ndoa au mahusiano yake. Maisha yako kwa mwanamke yanakuwa yapo rehani au yapo sokoni kama hutakua na silaha za kulinda penz lenu, Ili usimame vizuri katika ndoa au mahusiano lazima uhakikishe moyo wako umeshiba silaha hizi tatu nzito.
👉LOVE(UPENDO): Hakikisha moyo wako umeshiba upendo wa kweli, hii ni kinga yako ya kwanza katika ndoa au mahusiano na hata familia, moyo wako ukiwa umeshiba upendo wa kweli hakika nyumnba yako haitatetereka, mke wako hatokusumbua kwakua umeshiba upendo wa kweli, kila unachocheua ni furaha tupu. Kitu cha kwanza ambacho mwanamke anahitaji kutoka kwa mwanaume wake ni upendo wa kweli (True Love), Mwanamke anafurahi sana kuona upendo kutoka kwa mpenziwe, na huishi maisha ya kujiamini zaidi na uaminifu. Upendo huu tunaouzungumzia sio upendo wa maneno, Hakikisha unapenda kwa vitendo mtu akikwambia show love yan ni uonyeshe upendo kweli kweli.
👉CARE(KUTUNZA): Hii ni sector nyingine ambayo mwanaume unapaswa kuikarabati vyema ili uweze kusimamisha ndoa yako au mahusiano yako katika misingi imara, mwanaume unatakiwa ujue kumtunza mkeo au mpenz wako vyema. Niliwafundisha jambo moja kwamba usilalamike na kusema mkeo ni mbaya ukamchukia na kumdharau, Hakuna mwanamke mbaya maana akipata matunzo utamsahau, Ebu upe moyo wako jukumu LA matunzo ndani yako. Kumtunza mwanamke sio lazima umfanyie vitu vya gharama vilivyo nje ya uwezo wako hapana! Fanya kwa ule wastan wa hali yako ya maisha mbona atapendeza tuu, Unajua mkeo anatumia lotion hii mletee, unajua anavaa sendo size hii mletee usisubiri mpaka akuombe pesa ya kununua ebu mfanyie surprise ajiskie na yeye, akivaa sendo flan aseme kweli mme wangu anajua kuchagua hii ni yeye ameninunulia. Moyo wa mwanamke hulidhika sana na mambo madogo madogo.
👉CONCERN(KUHUSIKA): Kwanza hapa niwasihii wale wenye moyo wa ubinafsi, wajirekebishe kabisa. Mkeo au mpenzi wako anapokua anakushirikisha jambo lolote liwe la furaha au huzuni unatakiwa kuonyesha kujali au kuhusika, Moyo wako unatakiwa kupokea Jambo hilo na kushughulika nalo kama lakwako, Hii inampa tafsiri mwanamke kwamba upo karibu na yeye unatambua uwepo wake kwako na unaambatana na yeye. Kuna baadhi ya wanaume wanakuwa wakipuuzia mambo mengi tuu wanayoshilikishwa na wenzi au wapenz wao hii inampa mwanamke Hali ya woga na kutokujiamini, kuona kwamba hakubaliki.
J4REAL


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post