📂Usitake kila mtu aishi kwaajili ya kukufurahisha au kukupa furaha.
📂Usitake kumfurahisha kila mtu, wapendeze wale wanaopendezwa nawe.
📂Usitake kupendwa wala kusifiwa na kila mtu, Penda pale unapopendwa.
📂Usitake watu wote wapende unachofanya au wafanye unachopenda.
📂Chunga sana Sio kila kinachokuumiza wew basi na wengine kitawauma, unaweza ukawaeleza wakakuongezea maumivu.
📂Furaha ndogo uliyo nayo Imeushibisha moyo wako, usitake furaha kubwa zaidi kwa watu wasio na umuhimu kwako.
📂Silaha kubwa ya kuitunza furaha ya moyo wako ni wew kuishi sawa sawa na aina ya mazingira uliyopo, usitake kuwageuza watu vile wanavyoishi.
J4REAL
Post a Comment