Aliamka akiwa na uchu wa tendo la ndoa. Akaanza kumpapasa mkewe. Taratibu akainuka upande wake na kulala juu ya mkewe huku akianza kumbusu. Lakini mkewe hakuwa na ushirikiano kuonesha kuwa hakuwa tayari.
Mume akaendelea, akambusu shingoni, na kuanza kumtanua miguu..lakini mkewe akabana miguu zaidi. Mume akakasirika...
"Nini tatizo?" Mume akauliza.
"Sisi tuna matatizo" Mke akajibu.
"Unamaanisha nini? Mimi sikuelewi" Mume akauliza.
"Kitu pekee tunachoshirikiana vizuri pamoja ni tendo la ndoa tu" Mke akajibu.
"Nilifikiri unafurahia tendo la ndoa na mimi. Tizama nimekua muaminifu kwako. Sijawahi kukusaliti na wewe ni shahidi wa hilo. Sasa nini tatizo mpaka unanizuia?" Mume akamuuliza mkewe.
"Ni kweli. Unanifanya vizuri. Nafurahia. Lakini ndoa ni zaidi ya kufanya mapenzi. Haitoshi kuwa muaminifu pekee, ndoa inahitaji kuwa na kina, maongezi, mipango na mashauriano sio kufanya mapenzi. peke yake basi...
...Sipendi tuwe nafsi mbili ambazo zipo tupu. Nakumbuka mwanzoni mwa ndoa yetu, tulikua vizuri. Nahitaji tuongee, tucheke, tusali pamoja, twende out kama zamani, tukumbatiane, tutengeneze kumbukumbu, tucheze na watoto wetu na tutembee maeneo mbalimbali ili tuwe na intimacy katika ndoa yetu...
...Kitu ambacho tunacho sasa hivi sio ndoa, bali ni mipango ya kufanya mapenzi. tu. kufanya mapenzi. is just not enough" Mke akaongea kwa kulalamika.
"Ooh! Huu ni ukweli" Mume akajibu.
"Ukweli mchungu haswa" Mke akapigilia msumari.
Mume akaanza kupapasa nywele za mkewe taratibu na kuanza kuongea....
"Umeongea ukweli. Mambo yamebadilika sana tokea tupate watoto. Nafikiri ubize nao umechangia vivyo hivyo maisha yamekuwa tight sana."
Mke akamtaza mumewe na kuongea,...
"Darling watu hutengeneza muda kwa lile jambo lililo la muhimu. Kila jambo linalo wakati wake. Nahitaji niwe zaidi ya mama wa watoto wako tu, mimi ni mke wako. Nahitaji nijisikie kama mke wako na mwanamke wako unaenimiliki...
...Nahitaji muda wako mzuri kama uliokua ukinipa zamani. Sio mwingi. Kidogo tu. Nahitaji kupendwa nahitaji tuwe na maongezi. Nahitaji muda wetu wawili mimi ma wewe tu. Ni lini mara ya mwisho ulinipapasa nywele zangu kama unavyofanya sasa hivi?"
"Ni muda mrefu sana, hata sikumbuki ni lini". Mume akajibu.
Mke akaweka kidole chake kwenye lips za mumewe na akaendelea kuzungumza....
"Exactly, hujawahi kuchukua muda wako kunitizama kwa sababu kila siku upo busy tu. Unajua mwanamke haombi mambo mengi sana. Hata kitu kidogo tu kama hiki cha kunipapasa nywele zangu kinanigusa moyo wangu na kuona ni namna gani unavyonithamini...
Mke akaendelea....
...Wanawake wengi wamechoka na tendo la ndoa katika ndoa zao. Wana-fake orgasms, wanasingizia vichwa vinauma, wanasingizia kuchoka au hata kudanganya kuwa wako kwenye period ilimradi tu kukwepa kufanya mapenzi na waume zao kwa sababu hawajioni kama wanapendwa tena.
...Mimi nataka kupendwa mume wangu, sitaki kuwa kama hao wanawake. Hii nyumba yetu sio Lodge ya wewe kuja kulala, kufanya mapenzi na mimi na kuondoka. Hii ni nyumba yetu, kitanda chetu cha ndoa na tunayo ndoa halali kabisa..nakuhitaji mume wangu.."
"Nakuhitaji pia mke wangu, maneno yako yameniingia vilivyo. Ni kweli, muda pekee ninaokugusa ni wakati wa tendo la ndoa tu. Nimekua busy mno kiasi hata nimeshindwa kutafuta muda mzuri wa kuwa karibu ma wewe. Nakuahidi kuanzia sasa nitabadilika...
...Umenifundisha kitu cha muhimu sana, kwamba, watu hutengeneza muda kwa lile jambo lililo la muhimu. Wewe ni wa muhimu kwangu. Nitatengeneza muda wako. Muda wa watoto na muda wa kazi..." Mume akaongea huku akimsogelea mkewe na kumbusu.
Busu lilikuwa tamu, sio la haraka na sio la taratibu. It was intimate.
Mume akaweka kichwa chake kwenye kifua cha mkewe chenye joto kilichobeba maziwa mithili ya embe dodo mbivu. Na kwa muda kidogo wakaanza kuongea na kutaniana huku mke akichezea vidole vya mumewe.
Wakacheka pamoja, wakazungumza mambo mengi na hisia zao zikaunganishwa pamoja. Na bila kujielewa wakajikuta wakishiriki lile tendo takatifu lililo halalishwa kwao. Mke akampa mumewe haki yake kwa uhuru wote. Na mumewe akafurahia na kuburudika.
Kuanzia hapo, ndoa yao ikajengwa kwa msingi wa maelewano na wala sio s-ex peke yake. Na pale walipofanya s-ex haikuwa s-ex pekee bali ilikuwa ni Love making.
Post a Comment