✋Ni maumivu au raha gani unapata kuishi na mtu mwenye pesa nyingi, tajiri wa kutupwa anakupa kila unachohitaji lakin huna hisia nae au hana hisia na wew, mapenz yako kwake sio ya kihisia Bali ni kwasababu tuu anakupa pesa.
👉Pesa ni sehemu ya mahusiano tena huja automatically, ila mapenzi ni hisia. Unaweza kuwa na mtu mwenye pesa lakin mahusiano yako yakawa ya kutoa machozi kila siku.
👉Mtu anakuwa hana mapenzi na wew anakuwa na mtu wa watu wengi inamaana kama ni mwanamke pesa zikiisha anakuacha, kama ni mwanaume akikuchoka anatafuta mwingine.
👉Lakin mapenzi ni hisia unaweza kuishi na mtu ambae hana chochote ila ana mapenz yote kwako, mapenz yanayoshibisha moyo wako. Hakunyanyasi kwakua hana jeuri.
👉Kizazi cha sasa pesa imekua kipaumbele kwenye mahusiano, na ndio maana vijana wengi wanatendwa. Mtu anakwambia naishi na fulan kwakua ana pesa tuu nimchune lakin sina hisia nae.
👉Ishi na mtu kwa moyo na kwa hisia, Pesa zitakuja kutokana na upendo wenu. Usiishi na mtu kwa mapenzi ya pesa, hiyo ni dalili ya unafki na wizi.
J4REAL
Post a Comment