1. Usiharakishe kutoka nyumbani kwa wazazi wako kwa gia ya kwenda kuolewa.
2. Usimsubiri mwanaume mpaka aje ndio uanze kuishi. Unaweza kuishi maisha timilifu hata ukiwa huna mwanaume.
3.Achana na pombe zimewauwa wenzako wengi kwa kisingizio cha kuondoa stress na wewe unaweza kufa pia.
4. Usiwe mtu wa kuendekeza kuzipokea na kuzijibu namba ngeni za simu hasa nyakati za usiku.. sio njia sahihi ya kukupatia mpenzi....
5. Tengeneza mazingira ya kuilinda afya. Jitahidi Kunywa maji mengi na Chakula kwa diet achana na viofa ofa vya bure, vimesha waponza wenzio wengi mpaka sasa.
6. Vaa vizuri na kiheshima. Watu watavutiwa na wewe ulivyo kabla ya kuongea nawe.
7.Usitumie sex kama ndio mzani wa mapenzi. Unaweza ukaachika tuu pamoja na penzi lako taamu.
8. Usiolewe na mtu kwa sababu ya fedha; Utabakia kuwa mtumwa wake .
9. Jiongezee ubora wako, Tafuta kazi, Usiwe mpuuzi ukaamini mwanaume atatatua matatizo yako yote.
10. Jiheshimu sana kwa kuangalia namna ya uvaaji wa mavazi yako na mwonekano wako mbele ya jamii…. Usitegemee kuvaa kimini ukutane na mwanaume wa suti… wewe utampata wa milegezo na kubana pua tu.
Post a Comment