MAADUI ZAKO WAPO KARIBU YAKO - EDUSPORTSTZ

Latest

MAADUI ZAKO WAPO KARIBU YAKO


Hili somo nataka niwafundishe wafanyabiashara, kwasababu hili eneo lina maadui wengi kupita maelezo
.
Sikia unapoanza biashara jifunze kumtanguliza Mungu yani kuomba kwa ajili ya biashara yako, eneo lako la biashara, wafanyakazi wako, ombea mpaka wateja
Kwasababu kumbuka maadui zako ni wafanyabiashara wenzako, wao wapo wanaenda kuroga ili wapate wataje, wapo wanaenda kukuroga wewe ili usipate wateja na shetani hutumia sana hiyo mbinu ili na wewe ujiunge huko, uone kama Mungu huyu tunaemuabudu hana msaada wowote
.
Kuna maeneo yameisha laaniwa tangu zamani, kuna maeneo yamesemewa maneno mabaya mfano labda bila kufanya kitu flani huwezi kufanikiwa au lazima uwaone wazee fulani ndio utafanikiwa yani watu wanaroga ili wale kupitia kwako
.
Nini cha kufanya, kama wanavyoroga na wewe fanya hivyo hivyo, kwamba wanapita kwenye maeneo yao wakitupa uchawi wao, wewe ombea eneo lako la biashara huku ukilizunguuka na kumwagia damu ya Yesu, ukiona utaonekana unaroga kama wao, beba udongo nenda kauombee
.
Ukiona unashindwa, omba msaada kwa watumishi wenzako, au mchungaji wakusaidie kuomba na kuvunja nguvu za giza, maana vita ya ulimwengu wa Roho lazima ujipange ndio maana Neno linatuambia kwenye [Yakobo 4:7 Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.]
.
Wenzako wakienda kwa waganga wao wanatoa sadaka kwa ajili ya biashara zao, na wewe ukienda Kanisani toa sadaka maalumu kwa ajili ya biashara yako, yani unatoa huku ukitamka maneno unataka Mungu akutendee nini kwenye biashara yako
.
Kwasababu Neno linasema hazina yako ilipo na moyo wako uko hapo, kwamba mahali utakapotoa sadaka iwe kwa Mungu aliye hai, au kwa miungu, kumbuka ile roho ya ile madhabau itaambatana na wewe na kutimiza kile ulichotamka pale, ndio kazi kubwa ya Sadaka.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz