KWENU DADA ZANGU


-Najua ya kwamba unahitaji mume mwema atokaye kwa Mungu
- Najua kwamba moyo wako una shauku na kiu ya kuwa mama bora kwa familia yako
- Najua unatamani sana mwanaume ambaye atafanyika Baraka kwako na familia yako
- Najua unatamani kufanikiwa zaidi ktk NDOA yako baadae
- Najua wapo vijana unaowakataa kwa kigezo ya kwamba hawana mafaniko bado
- Najua kwamba huyo mchumba uliye nae unamuona ni wa low- class hajatatimiza vigezo vya kukumiliki
- Najua huyo unapenda kuolewa na mwanaume Mtumishi lakini hautaki kuacha tabia zako mbovu mbovu
Ngoja nikuelezw jambo;
- Ukitaka kilicho bora yakupasa nawe uwe bora zaidi ya kile unachokihitaji
- Ukitaka mafanikio ktk ndoa yako, anza kuonyesha bidii ya kazi angali upo nyumbani kwenu,, sina hakika kama lwenu umezoea kuwa golikipa halafu kwny ndoa uwe mchapakazi ni ngumu sana
- Ukihitaji mume mwaminifu, jitunze ww , anza kuwa mwaminifu kwnz tangu ukiwa nyumbani kwenu
- Ni gharama sana kupata kilicho bora
- Maisha yako Leo nyumbani kwenu, ni Taswira halisi ya maisha yako kwny ndoa yako
Wadada tubadilike, tuachane na tabia hzi mbovu mbovu ili Mungu apate kujibu haja za mioyo yetu
Mungu akukumbuke binti,, akufute machozi yako, na akujibu haja ya moyo wako
Nawapenda sana
Barikiwa
#Bintisayuni#
# Share#


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post