KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA SIKU HIZI


Ndoa nyingi hazina msingi wa Mungu namanisha nini;
Siku hizi watu wengi tunaingia kwenye ndoa kama fashion hatumshirikishi Mungu, kwa mfano unakuta mtu kwasababu anaona umri umeenda hajaolewa au kuoa anabeba yeyote tu ilimradi na yeye aonekane kuwa ameoa au kuolewa au kwenye historia naye aje kuhesabika kuwa aliwahi kuoa/kuolewa.
Wakati mwingine unakuta mtu anaolewa na Mwanaume au kuoa mwanamke ambaye ametafutiwa na rafiki yake au ndugu
Wawili hawa unakuta hawajapata muda wa kufahamiana vizuri na huyo mchumba wake,
Hajui strength mazuri au weakness/madhaifu za huyo mchumba.
Zaidi ya kuwasiliana tu kwa simu na kukutana mara chache .
Kwa style hii binti au mwanaume akiwa na madhaifu/ weaknes au tabia fulani sio rahisi kuzijua na kama utakuwa na hamu sana ya kuoa au kuolewa hata Mungu sio rahisi kumshirikisha hivyo hata yeye anakaa pembeni.
Sasa baada ya kuolewa au kuoana naye ndio unakuta kumbe oooh huyu yuko hivi na yeye anasema kumbe ooh uko hivii nakuishia kusema tu laiti ningelijua nisingeolewa naye au kumkubalia.
Kuna tabia ambazo unakuta mwenzako anazo na hukuzijua mapema katika hatua ya urafiki au uchumba na tabia hizo hazivumiliki kabisa katika ndoa.
That means ulibeba ubavu wa mwingine maana angekuwa ubavu wako ungeweza tu kuyavumila hayo unayosema hayavumiliki.
My take usikubali kutafutiwa mchumba na rafiki,au jirani hata kama umri umeenda kaa tu uvumilie uungoje wakati wa Bwana na yule ambaye moyo utamdondokea.Mimi wamekuwa wakinifuata wengi niwasaidie kuwatafutia huwa najiuliza huyu ana shida gani asimproach binti mwenyewe😀
Jambo la pili linalosababisha ndoa kuvunjika ni distant marriage (ndoa za blutooth)swala la kukaa sehemu mbalimbali kama mmeoana kwa kigezo cha kazi hii kwa sasa inasababisha cheating ktk ndoa almost 90percent nimeshuhudia kwa macho yangu.
Mwanaume akiwa mbali na mke wake na akatamani kufanya hilo jambo na mke hayupo he will do it with anyone hata kama ni mtumishi wa Mungu. (Ninao mfano hai)
Zamani ndoa za babu zetu, bibi zetu hawakuwa wanafanya kazi hivyo walikuwa wanakaa na waume zao muda wote lakini hii ya mke kufanya kazi Bukoba mme yuko Dar ni shida nina mifano ya ndoa nyingi ambazo zimepata shida kwa wao kuishi mbali mbali.
Mwanamke yeye anaweza kuvumilia kukaa muda mrefu bila kufanya tendo hilo na sio mwanaume.Ninawashauri wanandoa mnaoishi mikoa mbali mbali muangalie jinsi ya kufanya lakini msiendelee kukaa hivyo mtampa shetani nafasi.
Ndoa nyingine wanaoana kwasababu wametiana ujauzito na wanaogopa aibu kwa jamii au wazaz kushinikiza.
Sasa ndoa ya namna hii unategemeaje kama msukumo wa ndoa umeletwa na kupata ujauzito na sio upendo?
Wanandoa kuwa na ujuaji mwingi.
Kila mtu kwenye ndoa anajifanya anajua hakuna anayetaka kushuka.Ukiona ndoa nyingi zinadumu sio kwamba hakuna shida kwenye ndoa la hasha ila ujue kuna mmoja anayejishusha ili mambo yaende ,wote mkiwa wajuaji na wababe ndoa itawashinda.
Utandawazi.
Simu hizi zimeongeza rate of cheating zamani ili kumpata mtu muanze naye hizo process za uzinzi ilikuwa either mkutane ,au umwandikie barua hadi ifike huko hata hamu ya kuzini imeisha isha.
Lakini siku hizi bwana hizi simu mtu akishapata namba za simu tayari kila kitu wengi hufanya uzinzi hata kwa njia ya simu😳😳ndio msinishangae kwani uongo?
Mke/Mme kutokusimama kwenye zamu zao.
Wanaume hawawapendi wake zao kama kristo kristo alivyolipenda kanisa
Wake wahawatii waume zao kama kumtii kristo. Tumejichosha na kazi za kuajiriwa na kuacha majukumu yetu ya asili kwa wasichana wa kazi.
🤔Sasa mama kila kazi umemwachia housegirl
Kupika,kufua nguo za mmeo,kuandaa maji ya kuoga
Hadi kutandika kitanda hiyo ndoa akichukua huyo binti kweli utasema ni shetani?
Kutokuruhusu Roho Mtakatifu awe mwalimu ktk ndoa zetu,atufundishe,atuelekeze
Mimi najua ukiwa na Roho Mtakatifu atakufundisha jinsi ya kumuheshimu mme wako.
Jinsi ya kumpenda mke wako hata kama ana madhaifu
Jinsi ya kumwombea
Jinsi ya kumpikia
Jinsi ya kujibizana naye akiwa ana hasira and above all jinsi ya kukata kiuno kitandani
Ndoa nyingine ni adui anaziingilia sasa ukishajua ni adui huna haja ya kupambana na mme/mke wako pambana na adui
Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.(waefeso 6:12)
Wamama wengine tunaomba lakini michanganyo mingi anaomba akiona mme habadilik anaenda kwa waganga baadaye anarud tena kuomba
Wababa nao wengine hawawezi kuombea ndoa zao wakiona shida kwa mke wao wanataka tu kuchepuka badala ya kuwaombea woii.
Kukosa tunda la Uvumilivu unataka ukiomba sasahivi mda huo huo Mungu ajibu.
Tunasema tumeokoka lakini waume /wake zetu hawayaoni hayo matunda ya wokovu.
Mama unasema umeokoka lakini dharau kwa mmeo,kutwa unashinda kanisani nyumbani majukumu yako hufanyi,unamwabudu mchungaji wako lakini ukirudi nyumbani mme unamdharau.
Biblia inasema kwa matendo yako wewe mama mme anaweza kubadilika.
Je hayo matendo yako kweli yanamshawishi mme wako naye aokoke?
Kama ukirudi nyumbani umenuna humsemeshi eti kisa yeye hajaokoka hapo wokovu wako ni bure.
Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno (1petro 3:1)
Shida nyingine kubwa ni Soul Ties(Yaani vifungo)kama umeolewa na mwanaume aliyekuwa na tabia za kutembea na wanawake kibao huko nyuma zile roho za wanawake zimemfunga ,kila anapojaribu kuacha anajikuta tena anarudia kuzini ni kwasababu ya hayo Maroho ya hao wanawake aliowahi kuzini naye unahitaji maombi ya kumfungua katika hayo maroho ya hao wanawake wengine
Biblia inasema aziniye na kahaba ni mwili mmoja hivyo huyo mme/mke wako amefungwa katika miili ya makahaba wengi fanya maombi ya kumkomboa na kumfungua
Mambo mengine ni madhabahu unaweza kukuta umeolewa na mwanaume ambaye Baba yake alikuwa mzinzi au aumeoa wanawake zaidi ya mmoja uwe na uhakika kama usipofanya maombi ya kufunga hizo madhabahu za polygamist ujue naye either atazaa nje au ataoa mke mwingine au atakuwa penda penda.
Kama umeoa mke ambaye kwao kila anayeolewa anaachika basi ujue shida sio mke wako ni madhabahu za kwao zinamfuatilia kuvunja hiyo ndoa yenu.
Soma habari za Ibrahimu alizaa na kijakazi .Akaja mjukuu wake Yakobo akazaa na Vijakazi.
Hivyo katika kuomba Mwombe Roho Mtakatifu akufunulie atakuonyesha chanzo cha tatizo na ukishajua chanzo ni rahisi kudeal na hilo tatizo kwa msaada wake yeye mwenyewe
Wanaume acheni kuwa na tamaa,jifunzeni kuridhika na wake zenu.
Acheni kujichosha bure kila siku kubadilisha wanawake ,huyo mke wako ni mke mwema wewe mjali,mpe hela asuke,anunue nguo nzuri,ale vizuri ni mrembo sana huyo kuliko hao unaoenda kwao kila siku.
Hakuna mwanamke mbaya akitunzwa na kupendwa
Huko kwa michepuko hakuna jipya mtaenda kubeba tu magonjwa.
Wanawake jipende,jiamini wewe ni mzuri na wa thamani.
Huyo mme atarudi tu,endelea kuomba ,sugua goti Mungu anaenda kujibu atakurudia kwa magoti.
MUNGU ZIPONYE NDOA ZETU
Pastor W Kilemo


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post