KWANI MAPENZI YANATAKA NINI?

MAPENZI 😢
Yamefanya wengine wanawachukia wanaume pia yamefanya wengine wanawachukia wanawake
.,..
Mwanamke mmoja huko Benin amechakazwa vibaya na MTU anayedhaniwa kuwa ni Mme wake baadaya kutokea hali yenye utata dhidi ya watoto wao.
Mwanaume huyo tajiri na mfanyabiashara alikuwa na mpango wa kuhamisha family yake kutoka Benin kwenda Canada ndipo ubalozi wa NCHI hiyo ulipohitaji Vipimo vya DNA kwa watoto wake hao watatu kwa kuhofia kuwa huenda alikuwa akitaka kusafirisha watu wasiokuwa na uhusiano naye kinyume cha sheria (human trafficking).
Vipimo vilikuja na majibu kuwa bwana huyo siyo baba halali wa watoto wote watatu hivyo ufanyike utaratibu mwingine wa kupata Visa na taratibu zingine za kisheria ili aruhusiwe kuingia Canada.
Alirudi nyumbani kumhoji mke wake juu ya baba halali wa watoto hao na kwanini amekuwa msaliti kwa kiwango cha hatari kiasi hicho lakini hakupata majibu ya kueleweka.
Jamaa akaamua amuue kabisa lakini watu wakawahi kuokoa uhai wa mwadada huyo huku meno manne yakiwa yameng'olewa kwa ngumi nzito nzito alizosukumiwa.
Bado taarifa zaidi hazijatolewa kuhusu kukamatwa kwa mwanaume huyo lakini hali ya mwanamke ambaye ni msaliti ndiyo hiyo katika picha.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post