Wanawake wengi MNAAMBIWA na MNAAMINI kwamba namna nzuri ya kumfanya Mumeo akugande na sitoke nje ya ndoa labda ni kumpa kila anachotaka.
👆👆👆 Yategemea hapo Je imekugusa Neno la MUNGU 🙏 kwa hicho anachotaka
👆👆👆👆Yampendeza MUNGU Kwa hicho anachotaka
Na wengine kumpa mpaka mapenzi ya kinyume na maumbile wakiamini ndio njia sahihi ya kufanya aonekane wa thamani kwa Mumewe.
👆👆👆👆Hapo umejiloga mwenyewe 👌 ni dhambi kufirana 1Wakorintho 6:9
Ni CHUKIZO MBELE ZA MUNGU kufirana
👉 Wengine wamekuwa wakijifunza Zaidi mapenzi na style mbalimbali mpaka kunyonya sehemu za siri.
👆👆👆SIO DHAMBI NDANI NDOA NA SIO KOSA KIAFYA NDANI YA NDOA
Bali nje ya NDOA ni majanga nyonya Mkeo tu
Nyonya Mumeo tu bacteria rafiki hawasalitiwi
👉Wakati nakubaliana nao asilimia miamoja kabisa kwamba kujifunza na kujua vema namna ya kumpa penzi zuri mumeo ni moja ya kitu kitakachomfanya akuone wa thamani sana mbele zake lakini nataka nikupe vitu vingine amabvyo unaweza kuwa ulikuwa unavipuuza na kuchukulia vya kawaida lakini kumbe vina thamani na vina matokeo chanya sana kwa mumeo na huenda anatamani sana angefanyiwa lakini hawezi kusema👍🏾👍🏾
VIPO 10 TU ninavyokuletea LEO HAPA
❤️Mche Mungu na MUOMBEE Mumeo na uonyeshe mbele ake kwamba wewe unamtanguliza Mungu.
Hapa usifanye kwa unafiki ili uonekene lakini pia usifanye kwa kufichama,Labda nikuambie kitu Mume wako atathamini Kwa moyo wote unyenyekevu wako mbele za MUNGU 🙏 kama akikukuta uko busy pia unaomuombea kwa Mungu ABARIKIWE , AEPUSHWE na MAJARIBU ya ibilisi, na ukimuombea ulinzi , Mungu amtetetee na kumlinda na ukiombea NDOA yenu iwe yenye Baraka. Mwanaume atakusikiliza kisha atajua amepata Mke anaefaa sana.
😁😁😁😁👈
ONYO : Usiombe kwa unafiki kwa sababu umemuona anakuja basi unaenda kuanza kusali ili akukute ) hiyo haitampendeza Mungu , wewe ukiwa kweli mcha Mungu katika moyo wako basi lazima utakuwa muombaji mara kwa mara .
Na katika kuomba mara kwa mara lazima kuna siku atakufuma tu tena hutajua kama amekufuma maana hatataka ujue ila moyoni utakuwa umemuongezea kitu kwamba wewe ni mtu sahihi sana.
Lakini kikubwa ni hiki unapomuomba MUNGU anakusikia na anaikumbuka ndoa yako nakuibariki hapo utaona mafanikio sana tu🙏 Maana MUNGU ndio mwanzo na mwisho katika yote hivyo ukisali na kuomba basi lazima utafanikiwa katika uyaombeayo.
❤️ Kuwa msafi na nadhifu mwenye kupendeza wakati wote, MWANAUME hawezi kusema Mke wangu mbona huogi au mbona mchafu nguo umevaa chafu , bali moyoni atakuwa anatamani uwe msafi hivyo ni jukumu lako kuwa msafi , nadhifu na uvae mavazi ya kupendeza wakati wote ili hata ukienda mitaani asiaibike Mumeo. Mume anajiskiaje ukiwa mchafu afu anakuona mtaani na watu wanajua ye ndio Mumeo na ye yupo na wenzake we unapita mchafu basi anakuwa hajisikii vizuri. Jaribu kuwa msafi wakati wote miezi Miwili tu ujtaona kaanza kutamani mtoke out wote nakadhalika
❤️ Uwe MSHAURI na MFARIJI kwake . Wanaume wana mambo mengi ya kupambana na maisha katika shughuli mablimbali hata kama nawe Mke unafanya kazi bado Mwanaume ana majukumu Zaidi yako maana ndio anaeangalia familia yote hivyo ana mawazo na stress za maisha sana tu lakini Mwanaume mwingine atakuonyesha dhahiri kuwa anahitaji faraja yako na wengine huwa hawaonyeshi faraja .
Hapo ni jukumu lako kujua kuwa leo Mume wangu anaonkena ana stress sana labda kagombezwa kazini nakadhalika , hivyo umbembeleze kama mtoto maana ndipo walivyo Wanaume kama watoto tu 😃😃😃
Unambembeleza na atajisema tu kuwa amegombana na boss au na rafiki yake au kuna jambo hili na hili limetokea na limemkjwaza au linampa shida namna ya kutatua 👂👂👈🙏
Sasa wewe unaweza kuwa mara nyingi HUNA utaalamu wa mambo ya kazi za WANAUME ila unatakiwa uonyeshe kwamba una kitu cha kusaidia na ndio maana halisi ya Mke kuwa msaidizi (Mungu alimwambia Adam nitakufanyia msaidizi ili usiwe peke yako akampa Hawa )
SASA je Mwanamke unajua kuwa wewe ni msaidizi ❓
Lazima uwe na namna ya kumfariji kama mtoto vile😁😁😁👈❤️❤️❤️
Mwambie Mume wangu ❤️ Mungu akutie nguvu Mimi NAKUPENDA na NAKUAMINI na najua tutashinda tu licha ya kuwa jambo hili ni gumu bado tumeshapita mengi hviyo usiwaze babangu tutashinda tu.
Kasha kama ni ugomvi ndio tatizo lake basi unaingiza USHAURI wa kwamba apotezee na achukulie poa mueleze kwamba wewe ungependa kuona anakuwa hana ugomvi na mtu na ana Amani wakati wote ili nawe uwe na FURAHA .
Muonyeshe kiasi gani akiwa na huzuni nawe unakuwa na huzuni tena asana mueleze kwamba Amani yako inatokana na kumuona yeye akiwa na furaha na umueleze kuwa yeye ndio sababu ya furaha yako na hivyo unatamani nawe ulipe wema kwa kufanya uwe furaha kwake. hii pia inahusisha kumuaga vema na kumtakia mema anapoenda kazini na kwa Messages kumkumbuka .
Lakini pia akirudi akutane na Wewe mlangoni ndio umpokee begi na mizigo yoyote aliyo nayo na kwa kufanya hivyo anakuwa kila akitoka kazini kwanza na hamu kuja nyumbani lakini pia anatamani awe na zawadi au kitu chochote
❤️Jitoe kwa watu wengine kusaidia katika mambo mbalimbali kama vile MISIBA , HARUSI na MATUKIO mbalimbali ya kijamii, kwa kufanya hivyo utajenga sifa nzuri ambazo watu watampongeza Mumeo kwamba Mkeo ana roho nzuri , anasaidia wengine , anajitoa nakadhalika .
Mume atapokea kwa Amani sana pongezi anazopewa na kujiona yupo na Mke sahihi kabisa katika maisha yake . tofauti na akiwa anapita mitaani analetewa kesi za wewe kutukana wengine , kugombana na kuwachamba wenzio hapo ataona alipotea kabisa🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄
❤️Siku zote kaa kama msaidizi, yani hapa hutanielewa haraka ila ni hivi hata Mumeo akigombana na mtu we kaa upande wa Mumeo hata kama hayupo sahihi , akishitakiwa we kaa upande wa Mume tu, ukifika nyumbani utamueleza taratibu na mtaomba msamaha kwa mliemkosea lakini kamwe usikae upande wa anaegombana na Mumeo kisa umegundua Mumeo hayupo sahihi .
Yani we mtetee Mumeo kama vile mwanao ambavyo ungemtetea hata kama kakosa kasha ukifika nyumbani ukamtamjulisha yule mwanao kwa kosa ambalo mbele za wengine ulimtetea basi fanya hivyo kwa Mume mtetee kwa lolote , namaanisha wakimshitaki we simama upande wake ,wakimfanyia dhuluma simama upande wake, na katika lolote lile we uwe upande wake tu. Hata akigombana na ndugu zake au ndugu zako we msikilize Mume kasha mkitulia wawili utamshauri maisha yataendelea
Kwa kufanya hivyo unamfanya aone kuwa yupo na mtu ambaye yupo naye kwa lolote na unaweza baadae kumuambia kuwa alikosea hivyo mkaombe msamaha pale unapoona umemtuliza hasira zimeisha na atajua yupo na Mke sahihi. ( kuwa makini : kwenye baadahi ya mambo unaweza kukaa kimya ukaacha Wanaume wamalizane sio alazima uingilie ) walakini kama imekulazimu basi lazima uingie uwe upande wa Mumeo tu.
Kuwa msaidizi hasa kiuchumi msaidie Mumeo kwa kuomba kufanya kibiashara chochote ambacho unaona kinaweza kusaidia kumpunguzia mzigo wa majukumu, na pia katika mambo mengine ya kiusaidizi ya kawaida mbayo unaamini ndio usaidizi nayo ni kupika,kufua ,kuosha vyombo , usafi wa nymba nakadhalika
❤️ Mfanyie surprises za kuonyesha unamjali, hapa mfano katika vijisenti vyako unavyobana vikoba unaweza ukamnunulia shati zuri au suruali nzuri au nguo ya ndani au kitu chochote ama saa ambacho kitamfanya hata akiwa mbali akukumbuke kwamba ni Mke unayemjali sana katika maisha yake.
Kuna wakati bajeti inakataa na anaweza kujisema kwako kwamba hana pesa kabisa sio kwamba anataka msaada kwako ila we ndio pekee kwake ambapo akiongea anakuwa ametoa stress kidogo amefanya mzigo umekuwa wa kushuka , sasa kama una aka elfu 30 vikoba mwambie naweza kukuazima 30 kutoka vikoba , akisema fanya hivyo basio na ufanye kama alivyokutaka. Mume atajua niko na Mke mjanja kama nyoka na mwelevu kama ua anajua namna ya kunisaidia ninapokuwa sina ujanja .
❤️ Jitoe kwenye matukio ya ndugu zake na ya ndugu zako na uwapende wote nduguze na nduguzo pia, mfano SHEREHE , MISIBA nk ya upande wa Mumeo wewe unatakiwa ushiriki kwa uaminifu mpaka ndugu za Mume waone kuwa wakiwa na wewe mambo yanaenda hata kama ndugu yao hayupo yani kwa kifupi iiishi kama familia moja na ndugu wa Mumeo. ( onyo : simaanishi uwe unaenda kukesha kwa ndugu zake nyakati zote) hapa namaanisha katika ushirkiano wa mambo mbalimbali yanayowahusu wote mfano ndugu wa Mumeo ana mtoto anamaliza shule au chuo kama una uwezo na muda unaruhusu beba zawadi na ufike tena huku , Mume atashukuru maana atajihesabia kuwa amefika yeye huko , maana umemwakilisha ipasavyo
❤️Jiheshimu usiwe na michepuko kabisa wala tabia mbaya , Mume anapopata habari za kwamba sijui Mkeo jana hivi na hivi , leo hivi na vile , juzi hivi basi inafika kipindi anaona kama vile ngoja iwe ndio style ya amisha , naye anaanza kuwa hivyo ulivyo na hata Zaidi ya hivyo na hapo sasa akichepuka vibaya anaweza kuleta magonjwa na au ukamkosa Mume akaongeza Mke mwingine au akahama na kutafuta bibi mdogo .
(Onyo:hata kama unapata habari mabaya kwa Mumeo we usilipize yani we ishi maisha ya kawaida ya kumependeza Mungu na kufuata haya niliyokuambia naamini Mumeo ataanza kuona hakuna sababu ya kutoka nje itafika wakati ataona hakuna kipya anachopata akiwa nje badala yake kila jambo kwenye maisha linawahusu wewe na yeye tu) kwa kifupi uwe mvumilivu🙏🙏🙏
❤️ Jitahidi ujue namna nzuri ya kumridhisha na kumtosheleza kimapenzi , hapa jifunze huba na mahaba full , ili ukimpa mambo mwenyewe aone anamalizwa hamu ana anakuwa ametosha, yaani akatoshelezwa kabisa. Kila kinachowezekana kumfanyia kama sehemu ya kumridhisha kimapenzi fanya hivyo na uwe na ushirikiano hasa pale unapojua kuwa anataka.
( onyo : usifanye mambo yaliyo kinyume na maadili ili tu kumridhisha kamwe usifanye hivyo, maana kuna wanaoweza hata kumpa kinyume na maumbile eti ili wamridhishe hivyo haitakiwi kabisaaaa)Neno la MUNGU 🙏 Lina onya katika 1 Wakorintho 6 : 9 (Wafiraji/Walawiti hawataurithi Ufalme wa MUNGU) katika mapenzi kawaida kuna mambo mengi ambayo unaweza kufanya akajiona ametoshelezwa full , nadhani utatafiti mwenyewe kuhusu mambo hayo. Neno la MUNGU linasema katika 1Wakorintho 7 :34c
"Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii , jinsi atakavyompendeza Mumewe."
❤️Jifunze kusamehe na kupotezea baadhi ya mambo, Mwanaume sio Mungu kuna wakati atakukosaea akajua au asijue lakini wewe ndio unaeweza kuamua kuwa imara au kuzembea sasa kama utaamua kuwa imara basi jifunze kumamehe hata asipokuomba msamaha, na kwa baadhi ya mambo mfano alikutukana jana usiku asubuhi kukicha potezea amka mapema mpe haki yake , kisha muwekee maji ya kuoga mwambie karibu kuoga Mume wangu. Naye atapotezea kabisa habari ya jana na siku inakuwa njema au kama bado kuna kumbukumbu basi mwambie Mume wangu ninaomba unisamehe nakupenda na usiponisamehe sina Amani tena moyoni wewe ndio mfalme wangu my prince naomba please unisamehe, yani hapo hata kama alikosea yeye we muombe msamaha yani atajua kabisa kwamba alikosea lakini msamaha umeomba wewe yani atajibaraguza atajibu usijali Mke wangu nakupenda sana pia na hapo jioni atarudi na mboga nzuri au zawadi au kitu unachokipendaga Zaidi ili akufurashishe nawe maana atakuwa amejua kuwa umeamua kuwe na Amani katika familia.
Naamini kuna vitu umejifunza, kuna mambo huenda sijayaongelea lakini ni MUHIMU basi yaandike hapa chini kama comment za maoni yako na wengine watasoma na utakuwa umewasaidia sana lakini pia kwa ambacho bado hujakielwa vizuri unaweza kuuliza hapahapa chini kama comment Nani nitajitahidi kukujibu japo Niko busy mno.
KARIBU SANA
🔴 NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE 🙏
NA MALAZI YAWE SAFI 🙏
Post a Comment