Kuna tofauti kubwa kati ya mwanamke Msomi na mwanamke mwenye akili

Mabinti Poleni Sana na wanawake wasomi, mmeteseka sana kwa kusimangwa kuwa hamfai kuolewa na hamstahili kabisa, leo hii mwanamke akishasoma anaonekana kama mdudu, anakuwa kama mbwa asiye na mwenyewe, eti atatamani kumtawala mume, hivi wanaume tuna akili za nchi ipi?
Wanaume wasomi ni kundi jingine la watu wajinga.
Mwanaume msomi anatumia kiki ya usomi wake kumpata mwanamke tena kwa kujinadi "Nasomea degree ya 1 ya Udaktari"
Basi mwanamke anaona basi sio mbaya kwasababu ya usomi wake pengine ataweza kuiongoza familia na kuisimamia.
Taratibu maisha ya uchumba yaanza na hapo akiwa chuo mjanja kwa pesa za wazazi wake, chuo kikiisha ndipo balaa linaanza na ndipo ujinga wao unaanza kuonekana.
Mwanaume amekariri akishahitimu ni ajira jambo ambalo likishakwama kwake ni madudu tupu, mwanamke kwasababu yuna elimu ya kawaida basi atatumia nguvu ili kupa chochote kwaajili ya kuandaa maisha lakini mwanaume amekalia kusubiri ajira, mwanamke anajaribu kumshauri kuwa angefanya kazi fulani utasikia "Kazi hiyo ngumu mimi siwezi"
Mwanamke atasikia kuna kupakia matofali au mchanga kwenye lori atampasia huyu mwanaume lakini utasikia hiyo ni kazi ya wasio wasomi, wewe msomi unafanya nini? Pumbavu 😏😏
Basi nenda ukalime mwanamke akusaidie mtaji, nalo atasema siwezi, basi uje kwetu kuna kazi kwenye kampuni kusaidia mafundi wa kujenga kwa siku 7000, nalo utasikia siwezi hiyo kazi nitachafuka sana, mpumbavu wewe, usomi wako ni nini?
Leo mwanamke anaanza kuhaha, huyu ni mwanaume wa vipi? Je muda wa kumuoa ukifika ataweza? Kama ya kula tu binti akutumie? Hana vocha anasingizia anaumwa kwa mjomba apewe 20,000 eti ili atumie kwaajili ya vocha na Mb za WhatsApp.
Je kuna kuingizia shilling ngapi huko WhatsApp? Mpumbavu sana.
Inafika mahali hata wanawake wasomi wanakuwa na msaada kuliko udambu tunaoufanya wanaume wasomi wajinga.
Inafika mahali binti anaanza kuona unazingua akikuacha kwasababu hauna njozi unaanza kulalamika eti alikupenda ulipokuwa upo chuo ila kisa umekosa ajira anakuacha, hapana anakuacha kwasababu hauna njozi, umekuwa mtu tu usiyejua kesho yako uiwekeje?
Yaani haustahili, ukiona una akili kama hiyo usimtafute mwanamke ukamkwamisha mambo yake, mwanamume pambana iwe kuzibua mitaro au kupika sambusa, hata mchumba wako atapaona pakukutia moyo hata kupata tumaini kuwa ipo siku utafanikiwa.
Mimi mwenyewe Mtia Moyo nimekuambia, ukikwazika ujue inakuhusu, badilika wala sina faida kwenye mafanikio yako.
Hata usipocomment ukashare utakuwa umewasaidia wengi sana.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post