KUMPENDA MKE #KAMA KRISTO ALIVYOLIPENDA KANISA.
1. Tunapaswa kuwapenda wake zetu bila kujali mapungufu waliyo nayo. Kristo alitupenda tukiwa na maovu/mapungufu kibao.
2. Ni Upendo Wa kweli tu unaoweza kumbadili mke kutoka kwenye mapungufu/madhaifu aliyo nayo na kuwa mke safi.
Kristo alijipatia Kanisa safi lisilo na waa, KWA UPENDO.
Mwanamme usifikiri utambadili mke wako kwa kumfokea fokea hovyo na kumpiga.
Mke atabadilishwa na nguvu ya Upendo unaomwonyesha.

3. Upendo huu si Wa maneno tu, ila ni Upendo unaoambatana na TENDO.
Kristo alilipenda Kanisa hata AKAJITOA KULIFIA.
Sio kumtamkia tu kwa mdomo mkeo kwamba unampenda lakini mambo unayomfanyia hayaonyeshi Upendo hata kidogo.
Sio tu kuandika humu mitandaoni maneno matamu kwa mkeo kwamba unampenda, lakini matendo unayomtendea ni tofauti na ulivyoandika.
UPENDO HUU NI ZAIDI YA KUANDIKA NI ZAIDI YA KUTAMKA.

Si vibaya kuandika HUMU kwamba unampenda, ila ANDIKA KISHA TENDA ULIYOANDIKA.
Mpende kwa NENO na TENDO, huyo ni mfupa ktk mifupa yako, nyama ktk nyama zako.

Tumaini & Sarah Chanjarika (RWC)
Post a Comment