KILA MWANAMKE DUNIANI ANALILIA KUOLEWA KWA SABABU MOJA TU APATE MTU WA KUMJALI.

Image may contain: 2 people, people smiling, child and outdoor

Ndoa ni dhamana ya UPENDO ndo maana wanawake wamejikuta wanaishia kwenye MAHANGAIKO YA KI MAPENZI kwa kuaangalia kwamba awapo na NDOA furaha na Amani vitaishi nae na inapokuwa ndivyo sivyo INAACHA GHARIKA🌊 kwa maisha mengi ya wanawake😭😭
Mwanamke akimpata MUME amepata BABA na siku zote hakuna BABA atampa jiwe mwanae ikiwa ameombwa mkate🍞
Mwanamke kutanga na njia sio kama ni UCHAGUZI WAKE KUFANYA HIVYO ila ni wakati akijaribu kutafuta MWANAUME SAHIHI🎁
Majaaliwa ya MUNGU KWA MWANAMKE ni mtoto wakike kuwa chini ya Mwanaume, Kama wanaume wangefuata utaratibu wa UUMBAJI WA MUNGU kumhudumia MKE wala hivi vyuo vya HOTEL na QT usingeziona, ndo maana huko nyuma WANAWAKE wasomi na walojiajiri na kuajiliwa walikuwa wachache tena kazi zao kubwa ilikuwa NURSE, TEACHER lakini baadaye dunia kugeuka KILA MZAZI AKAMJENGA MTOTO WAKIKE KUSOMA kwa ajili ya kesho yake, Waswazi wanasema:-
 NGUVU YA MWANAMKE INATOKANA NA KIPATO CHAKE.
Japo nina tatizo na hilo, Kwa sababu Wanaume nao baada ya kuliona hilo WAMEGEUKA KUWA TEGEMEZI😂😂😂 na kulifanya tatizo kuwa pale pale Kwani MWANAMKE anataka MUME wakati huo huo MUME TEGEMEZI inakuwa balaaa tupu, Mimi nadhani kuliko KIPATO kuwa nguvu ya Mwanamke ni BORA kumjenga Mwanamke kuamini kwamba:-
 MWANAMKE AIJUE THAMANI YAKE ILI KUTOYUMBISHWA NA MIHEMKO YA MAPENZI.
Lakini kwa sasa haya yote yanajiri kwa sababu moja tu; ILI MWANAMKE AFURAHIE MAISHA NI LAZIMA AWE NA KIPATO CHAKE na mbaya zaidi na wanaume nao wanaegemea kwa Mwanamke mwenye MAHITAJI kama huna mahitaji wala huwezi kumpata Mwanaume wa kukubembeleza na msivyo na akili UNABEMBELEZWA KWA GHARAMA ZAKO😂😂 Maana wanaume wa sasa HAWATAKI MWANAMKE ASOKUWA NA CHANZO CHAKE CHA KIPATO kwani MILIMA hawataki ila MITEREMKO.
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria 🔨


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post