💓💓KAULI AMBAZO MWANAMKE HAPASWI KABISA KUZISEMA KWA MUME WAKE💓💓


💓Naendelea kukupa ushauri ili kuimarisha ndoa yako Leo nakueleza sentensi tatu kati ya sentensi nyingi sana ambazo hupaswi kumwambia Mume wako..
1. “MAMA YANGU ALINIONYA KUWA UTANIFANYIA HIVI.”💓💓💓
Sentensi hii inaweza kumfanya mmeo kuwaza mengi sana kuliko ulivyomaanisha wewe pale unapotaka kumkosoa kwa alichokifanya. Kwanza atagundua kuwa una watu wengi nyuma yako ambao wanakusaidia kumfikiria ‘hasi’ tena mbaya zaidi mama yako ambaye yeye anamheshimu sana.
2. “UNAFIKRA KAMA ZA BABA YAKO (UNAPOMKOSOA).”💓💓💓
Bila shaka unafahamu ni kiasi gani wanaume huwaheshimu na kuwaamini sana baba zao ambao wamewashauri mengi hadi walipofika hapo. Hata kama huwa anakueleza baadhi ya fikra au mawazo ya baba yake asiyokubaliana nayo, usidhubutu kabisa kumtolea mfano kumuonesha kuwa na wewe unamchukulia hivyo mzazi wake.
Kukosoana ni suala zuri katika maisha ili kurekebishana lakini angalia njia nzuri ya kupinga hoja ya mwenzi wako, kwa ustaarabu kuepuka kumkera.
3. “HIVI LINI UTAPATA KAZI MPYA..?”💓💓💓
Swali hili sio baya lakini kwa jinsi lilivyoulizwa lina kila dalili za kuleta shida sana kwenye fikra za mumeo/mchumba wako. Kwanza atajua ni kiasi gani unafikiria vibaya kuhusu maisha yenu hasa kiuchumi.. Ni bora kumwambia, “Mume wangu ninakuombea sana upate kazi mpya.” Ni ujumbe uleule lakini jinsi ulivyofikishwa unatofautiana sana.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post