Mara nyingi watu wakiongelea kuhusu mafanikio huangalia zao la mwisho la mafanikio, hawaangaliii nini kimeleta yale mafanikio. Hii ndiyo maana katika maisha wanaofanikiwa ni wachache kwani watu wengi wanakua wakitamani kufanikiwa lakini hawataki kufanikiwa. Unapopita mtaani na kuona Duka kubwa zuri la nguo unalitamani.
Unasema hapana na mimi nataka kufanya biashara, niwe mfanyabishara mkubwa wa nguo. Wengi watanagalia wateja wanavyomiminika katika Duka lile na kusema biashara ya nguo inalipa. Lakini watakaofanikiwa ni wale ambao wataangalia zaidi ya lile Duka la nguo.
Wataangalia tabu ambayo mhusika aliipata wakati anatafuta fremu, wataangalia namna alivyokua anasumbuliwa na TRA wakati anafungua. Namna ambavyo alikua anahangaika kuzungusha nguo kama mmachinga ili apate hela ya fremu, namna ambavyo wateja walikua wanaenda dukani kwake kujaribu nguo wanazitia majasho na wala hawanunui.
Wataangalia namna alivyokua akihangaika na mabasi kwenda kununua mzigo, namna alivyokua akilazimika kulala kwenye basi ili kubana hela ya Gest na anunue mzigo mkubwa, namna ambavyo wateja waliomuagiza nguo walizikataa kwakua zilikua haziwatoshi ikawa ni hasara kwake. Ndiyo wengi huangalia mafanikio.
Uzuri wa kuangalia mafanikio nikua hukupa munkari wa kutafuta zaidi lakini haukufundishi namna ya kutafuta hivyo. Ili ufanikiwe basi angalia changamoto na namna ya kuzitatua lakini ili usikate tamaa basi angalia na mafanikio. Kwa maana jifunze changamoto na zifanyie kazi lakini pale unapoona unakaribia kukata tamaa angalia na mafanikio ya wengine kama zawadi inayokusubiri ufanikiwe ili usikate tamaa.
Post a Comment