KAMA UNA WIFI MWENYE KIDOMODOMO BASI ASIKUUMIZE KICHWA MUAMBIE WEWE NI SHANGAZI TU!

Image result for UNATAKA KUJUA NI KWANINI WANAUME NDIYO HUONGOZA KWA KUTELEKEZA WATOTO WAO?
Dada mmoja alinipigia simu akiniambia kuwa ndoa imemshinda, nilimuuliza tatizo ni nini akaniambia kua tatizo ni mawifi zake ambao anaishi nao. Wanamfanyia mambo ya ajabu kiasi kwamba ameshindwa kuvumilia. Nilimuuliza vipi kuhusu mume wake anasemaje kuhusiana na hiyo hali. Anasema mume wake ni mpole sana na hawezi kujibishana na ndugu zake hivyo mara nyingi huongea kidogo na kumuambia vumilia.
Nilimuuliza Kama anaona kua mumewe anampenda, akasema kuhusu upendo wa mumewe hana shaka nao, nayeye pia anampenda lakini anashindwa kuvumilia ndugu wa mumewe hasa mawifi zake. Nilitabasamu kisha nikamuuliza nyumbani kwao Baba yake Mzazi wako wangapi, alishindwa kuelewa lakini alinitajia basi nikamuambia kabla sijamshauri chochote chakufanya aende kuwaangalia shangazi zake.
Hakunielewa lakini nilisisitiza, kwakua ananiamini alienda kuwaangalia na kunijibu kua ashawanagalia lakini hakujifunza chochote. Nilimuambia tena akawaangalie na sasa hivi aangalie mahusiano kati yao na Baba yake. Alienda kuwaangalia na baada ya kurejea aliniambia mambo makuu matatu kuhusiana na mahusiano kati ya shangazi zake wawili na Baba yake mzazi pamoja na familia yao.
(1) Wote Wameolewa Na Wanamaisha Yao; Nimara chache sana huonana kwa kutembeleana kwani hata wakifanikiwa kuja nyumbani Baba yao yuko kazini na Mama yao yuko katika biashara zake. Wameolewa na wanafamilia zao na nimara chache sana hutembeleana, inaweza kupita miezi sita hawajaonana ingawa wote wapo Dar, mara nyingi huonana kwenye matukio kama ugonjwa, misiba na sherehe, mawasiliano mengi ni kwa simu.
(2) Hakuna Ushirikiano Mkubwa Wa Kifedha; Baba yao ni mgumu sana kwenye pesa, hakuna kusaidiana sana, mara kadhaa wakikwama huja kuongea na Mama yao ili awakopeshe au awasaidie kuongea na Baba. Ingawa ni Kaka yao lakini Baba ana majukumu mengi ya familia yake na mara nyingi hawasaidii hivyo hulazimika kuongea na Mama ambaye mara nyingi huwasikiliza na kuwasiadia.
(3) Hawana Maamuzi Yoyote Kwao; Nishangazi zake lakini ni kama majirani tu, hawana mamauzi yoyote kwao kama watoto wa Kaka yao (Baba yake). Wao wanamsikiliza Mama yao kuliko wanavyowasikiliza Shangazi zao. Kwakifupi Shangazi hawana sauti yoyote kwao na ingawa Kaka zake wanafanya kazi, yeye kaolewa lakini hawawasiadii Shangazi zao kihivyo, msaada mkubwa wanautoa kwa Mama yao na si Shangazi zao.
Baada ya kuniambia hayo mambo matatu nilimuuliza sasa unachohofia ni nini kama mumeo anakupenda? Hao mawifi zako ndiyo watakua mashangazi wa watoto wako, miaka mitano tu ijayo hawatakua na kauli yoyote kwanu. Hata Kama mumeo angekua anawapenda na kuwasikiliza, anawasaidia kuliko anavyokusaidia wewe, lakini baada ya miaka mitano, watoto wenu wakianza shule, majukumu yakiongezeka atajali familia yake kuliko Dada zake.
Ndiyo wanaweza kuolewa, au wasiolewe wakazalishwa hapo nyumbani lakini mwisho wa siku mumeo hata kama anawapenda vipi hataacha kuwasomesha watoto wenu na kwenda kuwasomesha watoto wa Dada zake. Wape muda tu wa kuendelea kutamba sasa hivi mambo yakiwa si magumu, sasa hivi ndoa changa lakini baada ya muda mumeo atawaona mizigo, atawafukuza au atajifanya kuwatafutia kazi ili waondoke.
Baada ya muda sasa Kaka yao majukumu yakimzidi ataanza kuwakwepa, hatapokea tena simu zao na hatawapa misaada tena. Watarudi kwako kujibalaguza kwakua wewe ni wifi yao ili uongee na Kaka yao awasiadie. Ndiyo kama huamini haya wewe nenda kamuangalie Shangazi yako, kama huna Shangazi basi hata wajirani au rafiki yako. Ona namna mbavyo yeye na Baba yako wapo na uone kama bado Baba yako anampenda Shangazi yako kuliko anavyompenda Mama yako.
Kwa maana hiyo basi kama una mawifi wenye vidomodomo wewe waambie nyie ni Shangazi tu endeleeni kufurahia uwifi kwa sasa ila mkiishakua mashangazi mtakuja kulia shida kwangu na msijali nitaswaidia. Kisha mfuate mume wako muambie wala asiumizwe kichwa na maneno ya Dada zake, hawakusumbui kwani unajua watabadilika tu. Muambie unampenda sana na utondoka akitaka yeye na si mashangazi.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post