Inawezekana tayari unamchumba, inawezekana ndiyo unatafuta au tu una ndoto za siku moja utakua mke wa mtu. Kama ni hivyo basi ni lazima usome kitabu changu na hapa kabla ya kutoa elfu kumi yako nitakuambia kwa nini ni muhimu kwako kusoma kitabu hiki.
Kuna sababu kuu mbili za kwanza kabisa, ingawa kinahusu ndoa kwa ujumla lakini wewe ambaye uko kipindi cha uchumba unapaswa kujua mambo mawili. Kwanza kabisa ni kwamba mchumba wako akishakuoa atabadilika, yaani hayo mambo anayokuonyesha, zawadi anazokununulia na kukujali kote, miezi sita tu ya kwanza atakua mume wako na si mchumba, atabadilika.
Sasa kitu cha kwanza kabisa utakachokutana nacho katika sehemu ya kwanza ya kitabu changu ni kwanini atabadilika, hii itakusaidia kuacha kuona wasiwasi, kuacha kuichukia ndoa kabla ya kuianza. Kwani nikuhakikishie usipokua makini na mabadiliko ya mumeo, pia mabadiliko ambayo yatatokea kwako basi unaweza uharibu ndoa yako yote na kua mtu wa kulia tu.
Lakini jambo la pili nisehemu ya pili ya kitabu changu, hii itakufundisha namna ya kumfanya asibadilike. Miezi tisa ya kwanza ya ndoa yako ina umuhimu mkubawa wa kuamua aina gani ya mwanaume unayemtaka. Kwamba awe mwanaume wa kukupiga na kukunyanyasa kila siku au mwanaume wa kukujali na kukudekeza. Ukikosea hapo itakua ngumu sana kumbadilisha hivyo kama uunataka ndoa ni lazima ujue
Post a Comment