*KAMA KASHINDWA KUMJALI NA KUMHESHIMU MKE WAKO UNATAKA AKUJALI WEWE NI NANI?*



Image result for *KAMA KASHINDWA KUMJALI NA KUMHESHIMU MKE WAKO UNATAKA AKUJALI WEWE NI NANI?*

DOCTOR LOVE ❤

Ni ukichaa na upumbavu kwamba unatembea na mume wa mtu halafu unalalamika kuwa hakujali, unalalamika kuwa ukimuomba pesa anakupiga tarehe, unalalamika kuwa labda hakupendi anakutumia tu, unalalamika kuwa hajali hisia zako na hana muda na wewe. Kama unatembea na mume wa mtu na bado una malalamiko hayo basi akilizako niza Punda umebebeshwa mzigo mzito halafu unadhani umefugwa kwaajili ya kulishwa majani.

Dada yangu tayari ni mume wa mtu, yote anayokuambia kuhusu upendo anakudanganya. Hamna anachokupenda labda kwakua tu kitandandani unajihangaisha na unamlamba miguu kila siku ukidhani kuwa atamuacha mke wake. Hamuachi ndiyo maana pamoja na kumtukana mkewe kila siku, kumuita mshamba, kukusifia kuwa unajua mapenzi lakini mwisho wa siku anarudi kwa mkewe huyo huyo mshamba, mchafu hajui kupika!

Anajua kua wewe si mwanamke wa kuoa hivyo pamoja na ushamba wa mke wake hata siku akimuacha hatakuja kwako kwani hakuna mwanaume anataka mwanamke kama wewe. Siku ikitokea akamuacha mkewe ataenda kutafuta mwanamke mwingine anayejiheshimu si wewe. Hivyo badala ya kulalamika hakujali hembu ondoka nenda tafuta Kijana mwenzako muanze maisha.

Unalalamika kuwa vijana hawakutongozi, hivi unafikiri kuna Kijana mwenye akilia takufuata wakati anajua unapenda hela. Iko hivi mwanaume akiona unatembea na waume za watu anajua unapenda hela hata kama ni kama wewe huhongwi chochote hivyo watataka kukutumia tu basi. Narudia unakichaa kulalamika kuwa mume wa mtu hakujali, mtu kashindwa kumjali mke wake aliyemzalia kabisa.

Kadhindwa kumheshimu mkewe wa miaka kumi pamoja ambaye kila siku wanalala wote aje kukuheshimu wewe ambaye anajua kuwa huko kwake kimapenzi, ambaye akikuacha basi ni baraka na si laana. Acha ujinga Dada yangu, wewe danga tu na toa huduma bure lakini haimaanishi atakuja kukuheshimu au kukuthamini. Acha kulalamika na ondoka anza maisha yako, yaani unaiba TV ya watu halafu uananza kulalamika kuwa inaonyesha chenga! Unakichaa!



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post