Kuna watu wanakua na roho nzuri mpaka inaboa, ulikua na mahusiano na mtu, ulikua unampenda sana ukajitoa kwa kila kitu kwake, sasa yeye hakuona upendo wako, akawa anakunyanyasa, anakudhalilisha na hata kukupiga. Wakati anakufanyia yote hayo ndugu zake walikuona, waliona unavyovumilia, unavyoteseka na kunyanyasika, hata hukumuacha ukavumilia.
Lakini bado yeye akaja kukaucha tena kwa manyanyaso, ukaumiaweee, ukanyanaysika weee ukateseka wee na hatimaye ukapona maumivu. Sasa ukapata mtu wa kukupa furaha, unapata furaha tu mambo yanakunyookea unashanagaa ndugu na marafiki zake wanakuja. Wanakumabia baada ya kuachana na yule mtu eti maisha yake yamebadilika, amekua kama chizi hajielewi.
Labda starehe zimemzidi na hana uelekeo, wanakuomba umsamehe, urudishe moyo nyuma na yeye kulia kwako ni kila siku, anataka hata kunywa sumu kwaajili yako. Hapo kumbuka wewe una maisha yako, lakini ndugu na marafiki ndiyo wanaona umuhimu wako, wanataka urudie mateso, kwamba uachane na mtu wako sasa eti urudi akakupige tena!
Halafu hasa kwa wanawake unakuta unamuonea huruma unarudi unadhani kabadilika, hapana nikuambie kitu hajabadilika bali mambo yamemuwia magumu na wewe kakuona kama Kimbola chake. Hembu acha huruma za kipuuzi, huyo si mwanao si ndugu yako hivyo matatizo yake hayakuhusu.
Naomba nirudie mtu akiachana na wewe akirudi kwako akakukuta na mtu mwingine akitaka umuache mtu wako uje kwake huyo hakufai. Nimbinafsi na anajali fuaraha yake tu, tena ukilogwa ukimuendekeza basi atakuumiza kila siku kwani atajua kuwa huendi popote.
Kuna kusameheana katika mapenzi lakini kama tayari usha move on una mtu wako usigeuke nyuma, utamuumiza mtu wako anayekuthamini na utarudi kwa yule aliyekua anakunyanyasa na ukisharudi sio kwamba atakuthamini atakuhehsimu kwa muda halafu atarudi kukutesa. Acha huo ujinga muache apambane na hali yake!
Kwanza acha huo ujinga wakusema kama sijui umsaidie, huyo si ndugu yako wala nini, kama alikua anakupiga akakuacha na kwend akutafuta mtu mwingine huna wajibu wa kuhangaika naye. Hilo suala la kunyw asumu ni lake na ndugu yake na halikuhusu. Sasa unaweza kuw ana huruma ukasema umsaidie akakuharibia mahusiano yako ya sasa na akaja kukuacha.
Ushauri wnagu temana naye kabisa, kwamba waambie ndugu zake wawe karibu na ndugu yao lakini wewe huwezi. Acha kuruhusu mtu ambaye alishakua historia katika maisha yako akakuhaibia maisha yako, sasa anakunywa sumu inamaana utaishi naye kumsaidia mpaka lini,, kwmaba kama kila ukimkataa atakunywa sumu inamaana ndiyo uachane na mtu wako ili umbembeleze yeye.
Halafu huyo si yatima, amefiwa na wazazi yatimka ni mtu chini ya miaka 18 hivyo kkafiw atu na wazazi na hata kama angekua yatima si mwanao huyo acha kabisa huo ujinga wa kumuendekeza. Muambie kabisa huwezi kuwa naye endelea na maisha yako basi, acha kusikiliza sijui kafanya nini wlaa nini labda kama unataka kuharibu maisha yako endelea naye.
Unataka urudi akupighe akaakuue au!
Post a Comment