JINSI YA KUMKWEPA MWANAUME USIYE MPENDA NA ANAKUSUMBUA



Ishawahi kutokea kwa kila mwanamke ya kuwa kuna mwanaume mmoja ambaye anakutongoza ilhali unamchukia. Halafu mbaya zaidi ni kuwa mwanaume kama huyu haskii kabisa, kila ukijaribu kumkataa ndivyo anavyozidi kukuapproach.
Mara nyingi huwa inaanza hivi. Anakuapproach, anakutongoza halafu unamkubali kiasi cha kuwa unataka kumsoma akili yake. Baada ya kutoka out ama deti mara kadha ukakuja kugundua kuwa mwanaume kama huyu ana matatizo flani ambayo wewe binafsi hukuyapenda. Unajaribu kumkaa mbali lakini unamwona hataki. Unajaribu kila mbinu za kumtenga lakini yeye anasistiza.
Well. Wakati ni sasa wa kumwambia akuache kabisa kwa kutumia mbinu zifuatazo.
#1 Mwambie kwa upole kuwa hujiskii na yeye. Kama umegundua kuwa huyu mwanaume anayekuvizia ana matatizo lakini si tishio kwako, basi kumwambia ukweli ndio muhimu. Mwambie kuwa yeye ni mwanaume mzuri *hata kama sivyo*, lakini huko interested na yeye ndani ya moyo wako.
Akiuliza ni kwanini, mwonyeshe utofauti wenu. Unaweza kumwambia kuwa wewe ni mtu unayependa kuparty ilhali yeye ni mtu anayependa utulivu, ama unaweza kumwambia wewe ana uraibu flani ilhali wewe huna. Anaweza kuuliza iwapo munaweza kuwa marafiki, lakini iwapo unataka pia kuhepa unaweza kumwambia kuwa itakuwa vibaya kuwa marafiki kwa kuwa tayari mumeanza vibaya.
#2 Usijibu simu wala texts zake. Wakati mwanaume kama huyu amezuzulika na wewe, ama pia kuna wanawake wengine anaowaaproach, si lazima umpe maelezo kama ya hapo juu, bali unaweza kumwondoa polepole kwa maisha yako.
Kitu cha kwanza cha kufanya ni kuhakikisha kuwa haujibu simu zake wala kumtext hata kama umeboeka. Ukiwa unajibu simu zake basi utakuwa unampa matumaini kuwa uko interested na yeye. Ukimzima baada ya muda flani bila shaka atakuja kuelewa – ama unaweza tu kumpa ile hotuba ya kuwa wewe na yeye hamuingiliani.
#3 Mblock katika mitandao ya kijamii. Kando na kuwa hujibu sms zake wala simu zake, unapaswa kublock contacts zake zote katika mitandao ya kijamii ambazo unazijua. Kama unahisi kumblock utakuwa umevuka mipaka yakuonekana mbaya, na unaona si tishio kwako, basi angalau fanya kumdelete.
Kumuweka katika contacts zako kutampa hisia ya kuwa nyinyi wawili mna connection aina flani, aidha ya kibinafsi au kikazi, hivyo kuona kuwa ni haki yake kuwasiliana na wewe.
#4 Badilisha namba yako ya simu. Najua utahisi vibaya kubadilisha namba yako ya simu, lakini kama mwanaume atakuwa anaendelea kukupigia simu na kukutext mara kadhaa kwa siku, ilhali tayari amejua kuwa huko interested na yeye, basi itakuwa jambo la kufanya ili kujiokoa.
Pindi utakapojeuza namba yako, usijaribu kuiweka sehemu yeyote online, kwa sababu huyu mwanaume ama rafiki yake anaweza kuiona. Pia hakikisha kuwa marafiki zako hawapeani namba yako ya simu kwa yeyote.
#5 Jifanyishe kuwa una boyfriend. Wakati mwingine huyu nuksi akifikiria kuwa una boyfriend, atatulia na kuachana na wewe kabisa na kufuata mwanamke mwingine. Hii ni kweli haswa iwapo huyu nuksi ni mwanaume mwoga ama mwenye haya.
Ukianza kumwambia huyu mwanaume nuksi kuwa wewe hauko single, basi mwisho ataenda zake. Kama hatareact na hizi habari mpya, unaweza kutafuta mwanaume mwenye miraba halafu umfanye kuwa ni boyfriend wako wakati unamwona yuko karibu.
#6 Tafuta mbwa. Hili si jambo la haja kwa kila mmoja, lakini kama una kazi na uko na nyumba yako, na unasumbuliwa na wanaume aina kama hii, basi inakufaa ufuge mbwa. Ukiwa na mbwa mkubwa halafu mwanaume kama huyu afikirie kukutembelea basi atajipanga coz mbwa katika nyumba yako atakuwa akikulinda wakati wote.
#7 Safiri na marafiki zako.  Kama unaona mwanaume huyu nuksi anayatishia maisha yako, basi si vyema kusafiri ukiwa pekeako. Badala ya kusafiri pekeako, tembea mjini ukiwa na rafiki yako ama tembea ukiwa katika kikundi na rafiki zako.
Ili mradi usitembee pekeako wakati wote basi utakuwa umeponea kusumbuliwa na mwanaume aina kama hii.
#8 Tafuta barabara mbadala za kwenda shuleni, kazini nk. Kwa wale ambao wamezoea kutembea, ile barabara ya kawaida unayoitumia kutembea shuleni, kazini, ama katika shughli zako za kawaida zinaweza kukuelekeza moja kwa moja hadi kwa huyu mwanaume nuksi sehemu anakoishi, kazini ama sehemu ambazo anatembelea mara kwa mara. Kama anaweza kuwa na nafasi, anaweza hata kujiweka barabarani maksudi ili tu apatane na wewe.
#9 Vaa kofia na miwani. Kuvaa miwani na kofia wakati mwingine husaidia kujificha kutokana na mwanaume aina kama hii. Mwanaume huyu hawezi kukusumbua iwapo hataweza kukutambua wewe. So ni muhimu kuvalia hivi iwapo unaenda sehemu ambazo unaweza kutana na wanaume kama hawa.
#10 Mjulishe mwajiri wako na wenzako. Kama haijubi simu zake, wala kumtext ama online, kuna uwezekano mkubwa jamaa kama huyu kuweza kwenda katika sehemu  yako ya kazi. Kama unashuku kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kwake kuja sehemu unayofanya kazi basi ni bora zaidi kumjuliza mwajiri wako na wenzako ili wakati ambapo atajaribu kuja sehemu unayofanya kazi ataambiwa aende zake.
Bydaway, kama unadhania mwanaume kama huyu anayekusumbua hajui sehemu unayofanya kazi basi unakosea, wanaume kwa kawaida wana taaluma ya juu ikiha kwa kutafuta kile wanachotaka.
#11 Tafuta mwanaume mwengine akusaidie ili amalize mawasiliano yenu. Tofauti na wanawake, wanaume huwa wanareact haraka iwapo utawaomba usaidizi kama unasumbuliwa na mwanaume mwingine. Kama huyu mwanaume anakusumbua bila kukuacha basi unaweza kumwambia mwanaume unayemwamini haswa kama ni ndugu yako, mtu unayehusiana naye ama rafiki yako wa kiume.
Wakati wa kuchagua mwanaume kama huyu hakikisha kuwa ana uwezo mkubwa wa kushawishi ili aweze kumwambia huyu mwanaume msumbufu aachane na wewe kabisa. Hakikisha pia huyu mwanaume ana nguvu na uwezo wa kukabiliana na mwanaume kama huyu.
#12 Wahusishe polisi. Hii ndio suluhisho la mwisho kabisa na linapaswa kutumika katika hali zile nzito kabisa haswa kama umeona kuwa mwanaume kama huyu amekuwa tishio kwako na umejaribu kila hatua umeshindwa. Kama umeamua kuwapigia simu polisi jipange tayari kutoa ushahidi wote ambao utahitajika kama vile jumbe alizokuwa akikutumia.
So haya ndio mambo ambayo yanaweza kutumiwa kuhakikisha kuwa unakabiliana na mwanaume yeyote 


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post