.
1)Kuna watu wataanza na wewe wanakusaidia kufika mahali fulani Kisha wanaondoka kwa ajili ya kwenda kuwasaidia wengine. Wape Fursa ya kuwasaidia wengine pia, usiwe mbinafsi kuwang’ang’ania.
2)Kuna watu walikuja ili uwasaidie, wakishaimarika wanaendelea na Safari na wewe endelea na Safari. Usinung’unike kuwa hawako na wewe tena, Furahia mafanikio yao. Mungu alikutumia kuwasogeza hatua, usitake kuwamiliki.
3)Kuna watu walikuja kukufundisha Kitu fulani, ukishapata somo, wanaondoka. Inaweza kuwa kupitia maumivu ama furaha, ila somo utalipata. Wanakusaidia kukuongezea umakini katika maisha.
4)Kuna wengine walikuja ili wakuunganishe na watu wengine, wakishamaliza wanaondoka. Wanaweza wasikupe Kitu ila wakakuunganisha na Mtu/Fursa itakayokufanikisha.
5)Kuna wengine walikuja kukuharibia mwelekeo, wakishakutoa kwenye mstari, wanaondoka. Furaha yao na ushindi wao ni kuona umepoteza mwelekeo.
6)Kuna watu wamekuja kwa sababu kuna msimu mpya wa maisha yako, msimu huo ukishapita na wao wanakuwa wamemaliza kazi. Ni marafiki wa msimu.
7)Kuna watu walikuja kwa sababu kuna Kitu walitarajia kupata kutoka kwako, wakishakipata tu, wanaondoka. Hawana cha kukupa hawa, usijaribu kutarajia kutoka kwao.
Post a Comment