Dada zangu hembu acheni kujioa, narudia acheni kujioa. Najua mnafanya kazi, mna mishahara mizuri lakini tunasema jamaa kaoa kwakua kachukua majukumu ya mtu mwingine na kuyaleta kwake. Kama umeolewa lakini bado unajinunulia Pedi wewe umejioa Period! Hata kama unafanya kazi Mkiurugenzi Benki Kuu na mumeo Mlinzi jua kuwa ni kazi yake kukuhudumia wewe.
Nikiingia Inbox nina meseji zaidi ya elfu moja na sijui nitazijibuje ila karibu kila meseji ukifungua utasikia wadada wanalalamika eti mume wangu hahudumii familia, hatoi hela ya matumizi, halipi ada, sijui hawekezi katika ujenzi mimi ndiyo nafanya kila kitu! Sasa kama ndiyo unafanya kila kitu unamuita mumeo wa nini? Huyo ni kijana tu ambaye mnaishi naye!
Nimenza na mnaoingia kwenye ndoa kwakua ndiyo mnawalea hawa wanaume mpaka kuwa kama Dada zenu, eti kwakua una kazi unaona poa asipoleta hela, si unamshahara mnatumia wako unaisha ndiyo atoe vimatumizi unaona poa! Nikuambie kitu sasa hivi unaona poa kwakua majukumu si mengi! Unajishaua mimi siwezi kuomba mwanaume, najua huwezi kwakua si matumizi yenyewe ni Pedi, hela ya Saluni na vitu vingine vidogo vidogo.
Sasa hivi hutalia ila subiri mtoto atake kwenda shule na Baba yake anajifanya hana hela, mnataka kujenga hata muondoke nyumba ya kupanga anakuachia wewe kila kitu hapo ndiyo unaanza kulia kuwa hahudumii kumbe ulishamfanya mwanamke kitambo. Narudia cha kutoa matumizi kama mume hatoi arudi asikute chakula ndani, narudia wanaume wengi siku hizi ni Viazi hivyo ukimlea ana leleka.
Mapezni ni kusaidiana, tena si kusaidiana ni mwanamke kumsaidia mume na si kinyume chake, kama mshahara wake huuoni basi jua kuna mambomawili. Kwanza kuna mwanamke mwingine ana honga huko na wewe unalea familia au kuna sehemu anafanya mambo ya maendeleo kakuficha wewe unamlisha bure tu kama Mama yake!
Lakini kama mume wako ni Kiazi zaidi basi pesa zake zinaishia kuonyesha sifa kwa watu, kutoa kwa ndugu zake hata kununua bia kwa marafiki ili aonekane ana hela. Sasa wewe endelea kumlisha tu ila baada ya miaka mitano ushachakaa (Nautakaa kweli kwa stress za kujioa) atakuacha na kutafuta mpya na watoto atakutelekezea hutaamini na ujinga wako!
Najua mshaambiwa vumilia, sijui atabadilika ila kama umenitumia SMS inbox unalia kua mume hahudumii familia ni wakati sasa akirudi akute watoto washakula na hakuna chakula, akirudi hakuna umeme mkae gizani na akirudi akute watoto hawajaenda shule hakuna ada, kama halipi muambie basi wala asiumize kichwa watabaki tu hao nyumbani hakuna namna!
Nishamaliza kama ulitaka nikuambie tofauti sina majibu hayo, ni wakati sasa muache ujinga wakulea wababa wazima na wao kwenda kuharibu vitoto vya shule! Kama unataka kuambiwa vumilia atabadilika basi nawewe nikuambie vumilia atabadilika endelea kumlisha na akitaka hela ya Bia mpe kabisa! Hata akitaka ya kuhonga mpe usijali akifikisha miaka 75 atabadilika tu endelea kusubiri!
Post a Comment