🌹HAUHITAJI KUWA SAHIHI MUDA WOTE BALI KUWA MWENZI BORA KWA MWENZAKO❤️


Image result for 🌹HAUHITAJI KUWA SAHIHI MUDA WOTE BALI KUWA MWENZI BORA KWA MWENZAKO
Kamwe usije ukapoteza muda wako mwingi kutafuta mwenza aliyekamilika, badala yake jitengeneze wewe kuwa mwenza bora kwa mwenzako. Hakuna mtu aliyekamilika, bali watu wanaweza kuishi pamoja kama watachukuliana kwa mapungufu yao na kushirikiana kwa mazuri yao.
.
Kila mtu anapenda kukubaliwa kwa kile kizuri anachofanya, tumia tabia hii kwenye mahusiano yako ili kuyaboresha zaidi. Mkubali na kumsifia mwenzako kwa yale mazuri anayofanya, atafurahi na kufanya zaidi.
.
Siyo lazima uwe sahihi mara zote, wakati mwingine unahitaji kuacha kuwa sahihi ili tu muweze kuelewana na mwenzako. Furaha siyo kuwa sahihi wakati wote, bali kuweza kwenda vizuri na wengine wakati wote.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post