Eti Mimi ndio mume, wewe mwanamke dhaifu utaniambia nini? Nikisema nimesema sitaki nyongeza wala ushauri wako, kaa kimya.
Aliyekuambia kuwa mkeo ni mdhaifu nani? Na tena kuna wanawake wangekuwa single wangekwisha nunua magari yao ila walipojiingiza kwenye ndoa na mipango ikafia hapo, aliyeua ni wewe hapo na si mwingine.
Unamuoa mwanamke kafundishwa Biashara, ni mpambanaji, mhangaikaji, amefika kwako ni mwendo wa vigingi tu, akitaka biashara unamzuia, akitaka akalime unamzuia, pesa zote unatambea nazo wewe, mke ni kama house girl, hana hisa na pesa za nyumba, akilazimisha kujishughulisha akapata sijui laki 3, nazo kwa ubabe unapokea, siku 3 hazijaisha umeshahongea zote, ukiulizwa mkali hatari, eti wewe nani unipangie matumizi? Hutaki kwenda kwenu sikulei hapa, daaaah dunia tambara bovu.
Hizo ni kauli za kijinga na zimeshika hatamu hata kwenye ndoa za kikirsto, Aliyekwambia mwanamke ni mdhaifu nani?
Mwanamke si dhaifu kama mwanamume ulivyoelewa, Biblia inasema "Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu. 1 Petro 3:7
Elewa mwanamke ana akili kama wewe ni pengine anaweza kukuzidi, mara ngapi tumeona mwanamke akiwa wa kwanza kitaifa na kuna wanaume wanapata division zero?
Biblia inasema uishi na mke kama kitu kisicho na nguvu kwa mfano ukikaa jirani na glass au kioo lazima uwe makini hautarusha mawe, au ukibeba Mayai ni tofauti na ukishika jiwe.
Kwahiyo mwanamke ni kama trei ya mayai mikononi mwako tena unataka ukazungushe upate faida.
Kwahiyo mwanamke ni kama trei ya mayai mikononi mwako tena unataka ukazungushe upate faida.
Ukiishi hivyo na mke hakika faida yake ni kuvuuna upendo wake wote, huruma, kujali na kukusaidia kwa roho moja, shingo haitekwenda upande na atakuhurumia katika majukumu.
Amini kuna familia ni maskini kwasababu ya wanawake wa humo kunyimwa fursa za kuzarisha, na kubezwa kabisa.
Kwa leo naishia hapa ila ndio kwanza nimeanza.
Mtia moyo
Post a Comment