🔴🔴Kaa ukijua kabisa kwamba itafika kipindi katika maisha yake ambapo atagundua kuwa haukutakiwa kuwa sehemu ya maisha yake.
🔴🔴Ni kipindi ambacho atapata MOYO wa ujasiri wa kutokukusubiri na kukunyenyekea tena. Hatakusubiri tena umpigie simu au kuchukua simu yake na kukupigia.
🔴🔴Hatakaa tena kusubiri ufafanuzi wako wa uongo na excuses zako za uongo kwa sababu atagundua kuwa haustahili muda wake hata kidogo.
🔴🔴Ndio atalia sana kwa kuwa alikupenda toka moyoni, alijihakikishia kuwa wewe ndio mtarajiwa wale. Atabeba hisia zake zilizojeruhiwa mbali na wewe.
🔴🔴Kidogo kidogo ataanza kusahau na kuishi maisha yake japo kwa tabu mno. Atakuja kumpata mtu anayempenda. Atamfanya asahau maumivu yote ya huko nyuma uliyompa.
🔴🔴Ikifika kipindi hiko tafadhali, usimfuate na kuanza kuleta usumbufu eti unataka mrudiane. Ulipewa nafasi ukaichezea basi atleast muache na mwenzako afurahie maisha upande mwingine.
🔴🔴Nikukubushe Tu kama hukujua ni kwamba kisichomuua mtu, siku zote humkomaza kwa sana na humjenga upya
🔴🔴Kuwa na Busara walau japo kidogo, na thamini hisia za mwenzako. Mapenzi yanauma kwa kiasi kikubwa sana!
poleni dada zangu mnaokosa furaha amini fungu lako lipo tu.
poleni dada zangu mnaokosa furaha amini fungu lako lipo tu.
Post a Comment