Dada yangu kama unaingia kwenye ndoa basi jua mambo haya, uwe una pesa na kazi nzuri au ni Mama wa nyumbani jua mambo haya;


(1) Mume wako sio mtoto wakowa darasa la pili ambaye unamuambia sitaki ucheze na kina flani, sitaki uchelewe kutidi, sitaki hiki, sitaki hiki, sitaki kile. Mume ni mtu mzima na huwezi kumpangia kitu chochote, mume unaongea naye, mnaeleweshana, sipendi unavyoongozana na kina flkani unajua hivi na vile, kwanini usiwe unawahi hatawatoto wakuone, punguza pombe mume wangu zina madhara, mnaonea akikusikia hata asipokusikia poa ni mtu mzima kaamua huwezi mpangia!
(2) Mume wako sio Shoga yako mkigombana unaweza kumnunia mwezi hamuongei na vijembe juu insta, mume wako hawekewi status, mmegombana ongea naye, angalia na kitu chenyewe jishushe maisha yaendelee, unamnunia mwezi humpi unyumba kana kwamba wewe peke yako ndiyo unaweza kumpa labda mwanamke ukko peke yako, hapana hiyo sio ndoa, tumia mdomo kuongea na mume wako na si kuvimbisha mashavu!
(3) Mume wako sio jirani yako ambaye kila siku mnashindana naye, akifanya hiki wewe unafanya kile, akifanya hivi wewe unafanya vile! Mume akitoka an wewe unataka utoke, akinywa pombe nawe unataka unywe, akimpa Mama yake za wadi na wako unataka akupe, akichepuka nawe unataka kuchepuka.
Hapana, mume hushindani naye, kama unakunywa kunywa kwakua ni starehe si kwakua mume anakunywa, kama unamsaidia Mama yako msaidie kwakua ana shida si kwakua mume wako naye kamsaidia wakwake, kama unchepuka chepuuka kwakua ni tabia zako au una hamu zako lakini si kwakua unalipa kisasi kwa mume wako.
Ubaya wa kulipa kisasi nikuwa hakina raha mpaka yule unayemlipoa ajue na hapo ndiyo unapoharibu. Wanawake kabla ya kulalamikia waume zenu basi hembu timizeni majukumu yenu.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post