Katika maisha si watu wanaoamua thamani yako bali niwewe mwenyewe unaamua thamani yako. Kila mtu anaruhusiwa kuwa na maoni juu yako lakini tathimini ya miwsho juu ya wewe inakuhusu wewe tu na si mtu mwingine. Watu hawapaswi kukuamulia kama wewe ni Malaya, Mlevi au Masikini, hapana ni wewe unayemaua.
Watu hawapaswi kukuamulia kama wewe ni mpweke, una mazwazo mazuri au unafuraha, watu hawapaswi kukuamulia kama wewe. Una mwanaume au mwanamke anakuambia wewe ni mbaya na wewe unaamini, anakuambia umchafu unaamini na kujiona mchafu kweli, anakuambia amekusaidia kukuoa au kukubali kuolewa na wewe na wewe unamaini, anakuambia wewe ni masikini na unaamini!
Anakuambia huna akili, huwezi kufanya kazi unaamini unakaa tu nyumbani, anakushusha kwa kila jambo wewe unaamini. Labda nikuambie kitu kimoja, asilimia kubwa ya watu huona mabaya yao kwa kuangalia mabaya ya wengine. Kwamba mtu anapokuambia wewe ni mmbaya nikwamba ashajichunguza na kujiona kuwa yeye ni mbaya ndiyo akaona akushirikishe na wewe ili muwe wabaya wawili.
Hivyo kama mume wako au mke wako akikuambia wewe ni mbaya, wewe huna akili, huwezi kufanya kitu flani basi tabasamu lakini muambie hayo ni maoni yako ni namna unavyoniona mimi, sikukatazi kuniona hivyo lakini mimi najiona tofauti, kisha tabasamu tena na muonee huruma kimoyomoyo na ondoka zako.
Nenda kaafanye kitu kile kile ambacho alikuambia hukiwezi ili tu aone kuwa wewe sio yeye, yaani aone kuwa kwakua yeye hawezi kufanya kitu flani kwakua uwezo wake ni mdogo haimaanishi na wewe huwezi. Acha kuumizwa kichwa na maneno ya kejeli ya watu wengine, wewe ni bora kuliko hayo wanayosema na ukilijua hilo wewe basi inatosha.
Post a Comment