Kila simu upige wewe na akipokea mkiongea sekunde kadhaa utamsikia "Ngoja nitakucheki baadaye" kisha anakata simu halafu hakutafuti mpaka umtafute wewe au mpaka anapokuhitaji anapokuwa na shida flani ambayo anataka umsaidie au umtimizie.
Yuko online lakini hajibu meseji zako ingawa anachati na marafki zake.
Hawezi kuongozana na wewe wala kukusindikiza sehemu ila akikuhitaji anataka umsindikize tena anakupa taarifa wakati anaondoka hata sio masaa kadhaa kabla na usipoenda ni lawama na matusi.
Hakujali kwa chochote hata kukutumia meseji umeakaje lakini bado unajipendekeza kutuma mamia ya meseji.
Una matatizo gani? unakasoro gani? Hebu acha kumpa moyo wako mtu ambaye hata hakuthamini na kukupa muda wake.
sisemi akupende kama unavyompenda ikiwa mapenzi ni hisia lakini angalau akujali kama mwanadamu.
akupe hata muda wake kidogo.
Mtu wa namna hiyo ata ukifanikiwa kuingia naye kwenye ndoa ni sawa Kucheza bahati nasibu ili ushinde mamilioni ya fedha.
Post a Comment