PICHANI:Hawa Hassan akiwa na Diamond katika picha ya video ya wimbo wa Nitarejea |
Ukiachilia mbali wimbo huo lakini
pia stori kubwa ilikuwa ni mahusiano ya Diamond na Hawa,ikielezwa kwamba
walikuwa wapenzi wa muda mrefu tangia kipindi Diamond akiwa anauza mitumba
maeneo ya Tandale,hivyo watu walianza kuwatupia macho kwa karibu lakini ghafla
penzi hilo lilikufaa Mwanadada Hawa kupotea masikioni na machoni mwa wapenda
burudani.
Watangazaji Soud Brown na Kwisa
wanaoendesha kipindi cha Shilawadu kupitia Clouds Tv waliwahi kumtembelea
msanii huyo Hawa Hassan mara ya kwanza baada ya ripoti kuzagaa ya kwamba msanii
huyo ametopea katika matumizi ya vilevi hasa pombe za kienyeji(Gongo ikiwemo)
na kufanya naye mazungumzo ambapo msanii huyo alikiri kutumia Gongo.Baada ya
mazungumzo hayo Hawa alipata msaada na kufanikiwa kuacha kabisa ulevi ikiwa ni
pamoja na kuu nganishwa na Pilli Missana Sober House.
Lakini imeelezwa kwamba hali yake
imekuwa mbaya tena na ikizidi baada ya kupata tatizo la Ini ikielezwa kwamba
yawezekana ni kutokana na Ulevi.
Kupitia ukurasa wa Shilawadu,Soud
Brown aliandika;
“Dah... Nimemtembelea Dada Yetu
Msanii Hawa Kusema Kweli Hali Yake Mbaya, Tumbo Lake Kubwa Kama Ana Ujauzito wa
Miezi 9 Kasoro, Ana tatzo la Ini, mwili unajaa maji na inabd mara kwa mara
akatolewe Maji gharama ni kubwa mno kwa familia Yao”
Aliendelea kueleza tena;
“Hii ni mara ya Tatu Shilawadu
Wanakutana Na Hawa, Mara Ya Kwanza Mwaka Jana Ambapo Tulimkuta Akiwa Amebobea
Kwenye matumizi Ya Uraibu Aina Ya Gongo, Baada ya mazungumzo Hawa akakubaliana
na sisi kuwa Yupo Tayari.Kuachana na Matumizi hayo tukamuunganisha na pillimissanah_sober_house
Akasaidiwa kuacha na akaacha kabisa, Bahati mbaya Baadae Ameanza
kusumbuliwa na Ini (Huenda liliathiriwa na uraibu ule) Sasa Hv Hawa anaumwa
Sana, Halali ucku Mbavu zinamuuma”
Katika taarifa yake hiyo kwa Umma
wa Watanzania mtangazaji huyo alimalizia kwa kuandika;
“Dada Pili Misana Pamoja na Familia Ya Hawa wanapambana ili kuinusuru Afya Ya
Hawa, Watanzania, Wasanii Wenzake Na Wote mnaopata Taarifa hizi Tunawasihi
na Tunajisihi Tumshike Mkono Hawa... ”
Kutoa Ni Moyo Sio Utajiri,
Namba Ya Mama a Hawa Ni +255 762 31 35 87
Post a Comment