Kiungo wa Barcelona Ivan Rakitic anaamini Lionel Messi
hawezi kushinda tuzo yoyote msimu huu kwani ni lazima itaende kwa nahodha wa
timu yake ya taifa ya Croatia Luka Modric.
Modric ambaye katoka kushinda tuzo ya mchezaji bora wa
michuano ya Kombe la Dunia ya Golden Ball baada ya kuongoza taifa lake la
Croatia, Modric aliitwa Mchezaji wa Mwaka wa UEFA na ni mgombea wa tuzo ya
mchezaji bora kwa upande wa Wanaume wa FIFA.
Messi alipoteza nafasi ya kuchaguliwa, na mchezaji wa Real
Madrid amepigana na Cristiano Ronaldo na Mohamed Salah kwenye tuzo.
Rakitic anaamini Modric anastahili tuzo bora, na heshima
nyingine yoyote na mchezaji wake wa timu ya Barcelona Messi hawezi kushinda.
"Kama kuna tuzo ya pekee ambayo Lionel Messi hawezi
kushinda, basi hakuna shaka kwamba msimu huu inapaswa kwenda kwa Luka
Modric," aliiambia Marca.
"Haikuwa kushangaza kwangu kama angeweza kushinda na
kura nyingi zaidi. Huu umekuwa mwaka wake na nina furaha sana kwa ajili yake.
"Kama Messi sio bora, basi lazima iwe Modric."
Pamoja na kuiongoza Croatia katika fainali ya Kombe la Dunia,
Modric alisaidia Madrid kushinda Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.
Post a Comment