SOMA ALIVYOFUNGUKA MSUVA KUHUSU KICHUYA

Kiungo mshambuliaji Mtanzania anayekipiga Klabu ya Difaa El Jadida ya nchini Morocco, Simon Msuva, amepata taarifa za kiungo wa Simba, Shiza Kichuya kuwaniwa na TP Mazembe ya DR Congo na kumwambia ndiyo wakati huu aondoke Msimbazi.

Kauli hiyo, ameitoa hivi karibuni baada ya kupata taarifa za kiungo mkabaji wa Azam FC, Himid Mao, kutua Klabu ya Petrojet ya nchini Misri akiwa kama mchezaji huru.

Wakati Msuva akimpa mchongo huo Kichuya, tayari Kichuya ameongeza mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Simba kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Akizungumza na Global Tv Online, Msuva alisema anafurahia kuona idadi ya wachezaji wa hapa nchini wakipata ofa za kwenda kucheza nje ya nchi kama ilivyokuwa kwake, Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu, Farid Mussa na Himid.

Msuva alisema, anaamini Kichuya ana uwezo wa kucheza nje ya nchi ikiwemo Congo kwenye timu ya Mazembe ambayo imeonyesha nia ya kumsajili, hivyo ni wakati wake wa kutoka nje ya nchi kwenda kutafuta changamoto mpya.

“Nimepata taarifa za Kichuya kuhitajika Mazembe kwa ajili ya kwenda kucheza soka la kulipwa, niseme ni nafasi nzuri kwake kwenda kutafuta chagamoto nyingine mpya nje ya nchi.

“Ninafurahia kuona idadi ya wachezaji ikiongezeka ya kwenda kucheza soka la kulipwa, hiyo itatusaidia sisi kuitangaza nchi na kuwavutia mawakala na kuja kuchukua wachezaji wengine.”

“Nimefurahia kuondoka kwa Himid hapa nchini na kwenda kujaribu changamoto Misri yenye ligi ya ushindani, hivyo kutasaidia kutengeneza timu bora ya taifa.

Simon Msuva

“Kwa Kichuya kuondoka ni muda muafaka ameshafanya mambo makubwa hapa nchini, hata kama atakwenda timu nyingine lakini iwe nje ya Tanzania, ingawa ukweli ni kwamba nje''

kuna changamoto nyingi sana lakini ukiweza kukubiliana nazo unafanikiwa na ni vyema aondoke umri ukiwa mdogo,” alisema Msuva.

 Msuva amesema hivyo siku chache baada ya kudaiwa kuwa Kichuya ameongeza mkataba mwingine wa miaka miwili na timu yake ya Simba baada ya ule wa awali kumalizika.

Ilikuwa inadaiwa mara kwa mara kuwa Kichuya anakwenda kucheza soka la kulipwa nchini Morocco au timu moja ya Afrika Kusini ilikuwa inamtaka lakini bado aliamua kukubaliana na Simba na kusaini mkataba mpya wa kubaki kwenye timu hiyo ya Msimbazi ambayo itashiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika kuanzia mwishoni mwa mwaka huu.

Hata Hivyo, bado Kichuya anaweza kwenda nje wakati wowote kwa kuwa inaelezwa mkataba wake unamruhusu kuondoka Simba wakati akipata timu.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post