KOMBE |
Ikiwa zimesalia siku kumi tu mataifa 32 kuanza kucheza fainali za 21 za kombe la dunia huko nchini Urusi, vikosi vyote wameanza maandalizi kujinoa vikali na michuano hiyo na wameonesha ubora wa hali ya juu lakini je nani kuibuka kidedea na kupokea kijiti kwa timu ya taifa ya Ujerumani kwa kubeba kombe hili lenye ubora na hadhi ya juu duniani?
Miaka ya 80 na 90 timu kutoka bara la America (Brazil na Argentina) walikua na vikosi bora hivyo haikua ajabu kubeba kombe hilo mara kwa mara hata hivyo upepo ulikuja kubadirika ghafla na ufalme huo ukahamia ulaya timu za Ujerumani, Hispania, Italia, zikiimarika na kufanya mapinduzi makubwa kisoka hivyo kuwapa mtihani mgumu timu kutoka bara la America, Asia na kwingineko kuchukua taji hilo.
Ndani ya fainali kumi zilizopita katika michuano hii ya kombe la dunia, takwimu zinatuonesha matokeo yafuatayo :
Fainali za mwaka 1978. Mwenyeji wa fainali hizi alikuwa ni Argentina, alifanikiwa kumfunga Uholanzi 3-1 ndani ya dakika 90 hivyo kubeba kombe hilo kunako ardhi ya nyumbani kwao
Fainali za mwaka 1982. Zilifanyikia nchini Hispania, huku Italy akiwa bingwa kwa kumfunga Ujerumani 3-1 fainali.
Fainali za mwaka 1986 zilifanyika nchini Mexico na ni Argentina tena aliibuka shujaa nakubeba kombe safari hii akimfunga Ujerumani mabao 3-2.
Fainali za mwaka 1990 Italy akiwa mwenyeji wa michuano hiyo tulishuhudia Ujerumani ikibeba kombe kwa kumfunga argentina goli 1-0
Fainali za mwaka 1994 zikipigwa kule Marekani, ni Brazil walifanikiwa kubeba kombe wakimfunga Italy kwa mikwaju ya penalty 3-2 hii ni baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya bila kufungana
Fainali za mwaka 1998 kule Ufaransa zilishuhudia mwenyeji timu ya Ufaransa akiwa bingwa kwakumfunga Brazil mabao 3-0
Fainali za mwaka 2002 nchi mbili zilikua mwenyeji (Japan na Korea kusini) na si wengine ni Brazil alibeba kombe safari hii akimfunga Ujerumani goli 2-0
Fainali za mwaka 2006 zilifanyikia ujerumani, tukashuhudia Italy akiwa bingwa alimfunga Ufaransa kwa mikwaju ya penalty 5-3 baada ya dakika 120 kwenda sare ya goli 1-1
Fainali za mwaka 2010 kwa mara ya kwanza zililetwa bara la Afrika kule Afrika kusini huku zikishuhudia Hispania kuwa mabingwa wakimfunga Uholanzi goli 1-0 ndani ya dakika 120
Fainali za mwaka 2014 zilifanyika kule Brazili, si wengine bali timu ya Ujerumani ilimfunga Argentina katika fainali goli 1-0 na kubeba kombe hilo
Hivyo katika historia ya michuano hii nchi ya Brazil iliyopo katika bara la Amerika inaongoza kuwa na mafanikio kwakulibeba kombe hili mara tano ikifuatiwa na Ujerumani iliyopo bara la ulaya kwakubeba mara nne hata hivyo ndani ya miaka kumi kama nilivyokuonesha takwimu.
Ulaya wamebeba mara sita na Amerika mara nne tu na kwa upepo unavyovuma naimani kombe linakwenda ulaya tena mfululizo hivyo kuwa la 7 katika miaka kumi maana vipaji na ubunifu ukiongeza na soka la ushindani vimehamia ulaya na majina ya mtu mmoja mmoja vimebaki kwa timu za amerika
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au
kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Post a Comment