Mbunge wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee |
HATMA NA MAAMUZI YA HAKIMU KUHUSU KEZI YA HALIMA MDEE
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa ahirisho la mwisho katika kesi inamyomkabili mbunge wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee ya kutumia lugha ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli
Hayo yamesemwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambaye leo ametoa ahirisho hilo la mwisho kwa upande wa mashtaka baada ya wakili wa Serikali mwandamizi, Patrick Mwita kudai kesi ilipangwa kwa ajili ya kuanza kusikilizwa, hawana shahidi ikiwa ni mara ya tatu.
Hakimu Simba amepanga kesi hiyo kusikilizwa tena Juni 29, 2018 kwa mashahidi wa upande wa mashtaka kuanza kutoa ushahidi.
Mdee anadaiwa kufanya kosa hilo Julai 3, 2017 Makao Makuu ya Chadema yaliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni ambapo anadaiwa kutoa lugha ya matusi kwa Rais Maguifuli kwa kusema "anaongea hovyo hovyo, anatakiwa afungwe breki kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au
kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Post a Comment