YALIYOJILI EPL SIKU YA MWISHO LIGI KUU ENGLAND



Mohamed Salah alivunja rekodi ya ufungaji mabao katika Ligi Kuu ya England baada ya kuwafungia Liverpool mabao 38 michuano yote msimu huu.

Hilo ni moja tu kati ya matukio muhimu yaliyotendeka siku ya mwisho msimu huu wa 2017/18 Ligi ya Premia Jumapili.

Mabao ya Salah yaliwasaidia Liverpool kufuzu kwa michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao.

Bao la Salah la 32 ligini msimu huu lilimuwezesha kuwapita Alan Shearer, Cristiano Ronaldo na Luis Suarez. Dejan Lovren alifunga kwa kichwa, Dominic Solanke akafungia Liverpool bao lake la kwanza naye Andrew Robertson akafunga jingine na kukamilisha ushindi wa 4-0 wa klabu hiyo ya Anfield dhidi ya Brighton.

Klabu hiyo ilikuwa inahitaji alama moja pekee kuwapita Chelsea na kujikatia tiketi ya kucheza ligi hiyo kuu ya klabu msimu ujao.
Chelsea kwao ni Europa League

Chelsea, waliopokezwa kichapo cha kushangaza na Newcastle sasa watacheza Europa League baada ya kumaliza nafasi ya tano.

Ushindi wa Liverpool hata hivyo haukutosha kuwafikisha nafasi ya tatu kwenye jedwali ambayo ilitwaliwa na Tottenham waliopata ushindi wa 5-4 dhidi ya Leicester kwenye mechi ambayo huenda ikawa yao ya mwisho kuchezea Wembley kama uwanja wao wa nyumbani kabla ya kuhamia uwanja wao mpya White Hart Lane.
Mohamed Salah alitawazwa mchezaji bora wa Ligi ya Premia Jumapili

Vijana hao wa Mauricio Pochettino walijipata nyuma mara tatu, lakini Erik Lamela na Harry Kane walifunga mabao mawili kila mmoja, Kane akifikisha magoli 30 ligini, naye Christian Fuchs akajifunga na kuwapa ushindi.

Mwenzake Kane katika timu ya taifa ya England Jamie Vardy alifunga mabao mawili pia siku hiyo lakini upande wa Leicester.

Iwapo Liverpool wangeshindwa na Brighton, bado hawangekosa nafasi ya kumaliza katika nafasi ya nne baada ya Chelsea kulazwa 3-0 ugenini Newcastle.

Ayoze Perez alifunga mabao mawili baada ya Dwight Gayle kufungua ukurasa wa mabao na kuhakikisha Newcastle wakiwa mikononi mwa Rafael Benitez walimaliza nafasi ya 10 kwenye jedwali.REUTERS

Vijana wa Antonio Conte nao walilazimika kuridhika na nafasi ya tano, macho yao kwa kiwango kikubwa yakiwa kwenye fainali ya Kombe la FA Jumamosi dhidi ya Manchester United.

Swansea walihitaji kushinda, Southampton nao washindwe na Man City na kuwe na mabadiliko ya tofauti ya mabao kwa magoli 10 ndipo wanusurike.
Rekodi ya alama 100

Swansea waliongoza dhidi ya Stoke lakini mwishowe wakashindwa 2-1 na kushushwa daraja hadi ligi ya Championship msimu ujao.

Gabriel Jesus alifunga bao dakika za mwisho mwisho na kuwapokeza Southampton kichapo na kuwakabidhi mabingwa wapya Manchester City ushindi waliohitaji kumaliza msimu wakiwa na alama 100, ambayo ni rekodi.

Mechi ya mwisho ya Arsene Wenger akiwa Arsenal, baada ya kuwaongoza kwa misimu 22, ilimalizika kwa ushindi kutokana na bao la Pierre-Emerick Aubameyang kipindi cha kwanza lililowapa ushindi ugenini Huddersfield.Manchester City waliweka rekodi ya mpya ya kumaliza na alama nyingi zaidi EPL msimu wa 2017-18

Mashabiki wa timu zote mbili walimshangilia Wenger dakika ya 22 ya mchezo na ndege mbili zilipaa juu ya uwanja zikiwa na ujumbe wa kumuunga mkono na kumshukuru Mfaransa huyo.

West Brom walinusurika kusalia Ligi ya Premia na walikamilisha msimu kwa kulazwa 2-0 ugenini Crystal Palace, kutokana na mabao ya Wilfried Zaha na Patrick van Aanholt.

Katika mechi ambayo timu zote mbili zilikuwa chini ya mameneja wa zamani wa timu pinzani, West Ham wakiwa na David Moyes waliwashinda Everton wakiwa na Sam Allardyce, Manuel Lanzini akifunga mabao mawili kufanikisha ushindi wa 3-1.
Ushindi kwa Manchester United

Marcus Rashford alifunga bao pekee na kuwawezesha Manchester United kushinda 1-0 nyumbani dhidi ya Watford, na kwingineko Callum Wilson alifunga bao dakika ya 93 na kuwawezesha Bournemouth kujikwamua na kushinda 2-1 wakiwa ugenini kwa Burnley.

Nchini Scotland, Rangers na Hibernian walifunga mabao 10, kila timu ikifunga mabao matano na kutoka sare ya 2-2 uwanjani 10 Easter Road.Manchester United walishinda mechi 21 za EPL msimu huu ambazo walitangulia kufunga. Ndio wa pili kufanya hivyo msimu wa EPL baada ya Portsmouth i2007-08)

Hibs walijipatia uongozi wa 3-0 dakika 22 za kwanza lakini Rangers wakasawazisha kufikia wakati wa mapumziko.
Wageni Rangers walionekana kuwa mbioni kupata ushindi walipoongoza 5-4 mechi ikisalia na dakika tano lakini Jason Holt alifukuzwa uwanjani na Jamie Maclaren akafunga bao lake la tatu na kuwawezesha Hibs kupata alama moja.

Aberdeen nao waliibuka kuwa timu ya kwanza ya Scotland kuwalaza Celtic ambao wamekuwa chini ya Brendan Rodgers. Aberdeen walifanikiwa kumaliza wa pili ligini nao Rangers wakamaliza wa tatu.


EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post