Italy ilitolewa na korea kusini kwenye kombe la dunia mwaka 2002 lililoandaliwa na nchi mbili japan na korea kusini.
kwenye hatua ya mtoano italy ilipangwa na wenyeji wa mashindano hayo korea kusini mechi ambayo ilipangwa kuchezwa katika mji wa Daejon nchini korea kusini huku refarii wa mchezo huo akiwa ni byron moreno Raia wa Ecuador mwenye asili ya kikorea.
Hilo ndo jina ambalo linaweza kuongozwa kwa kuchukiwa na waitaliano kutokana na maamuzi ambayo aliyatoa kwenye mchezo huo.
Mchezo ulienda kwa sare mpaka dakika 90 ambapo sheria iliruhusu kwenda kwenye dakika 30 za nyongeza ambazo zilifahamika kama (golden goal) .
Sintofahamu inatokea kijana Ahn jung-hwan anaipeleka korea kusini robo fainali, kwa kuifunga italy katika dakika hizo za dhahabu.
Ila kituko zaidi ni kwamba Ahn jung-hwan alikuwa anachezea klabu ya perugia ambapo ilikuwa seria B kipindi hicho baada ya kuwafunga goli kombe la dunia italia mchezaji huyo alivunjiwa mkataba na klabu hiyo. sababu kubwa ni kuchukiwa na taifa la italy kwa sababu asingeweza kuishi italia kwa furaha.
Post a Comment