Time ya watoto wamitaani toka Tanzania |
Mashindano ya Kombe la Dunia la Watoto yameendelea tena mjini Moscow nchini Urusi katika uwanja wa klabu ya Lokomotive Moscow ambapo michezo ya nusu fainali ilichezwa ambapo timu ya wasicha waishio katika mazingira magumu kutoka Tanzania ilipambana na Uingereza na mwisho wa mchezo Tanzania imefanikiwa kutinga fainali kwa kishindo kwa kuibamiza na kuisambaratisha bila ya huruma timu ya Uingereza kwa magoli 2-1 huku Magoli yakifungwa na mlinzi Mastura Fadhili na
Mshambuliaji Asha Omari
.
Timu ya Tanzania street Academy na viongozi wa timu pamwe na maafisa ubalozi wa Tanzania nchini Urusi
Tanzania itacheza fainali na Brazil kesho kutwa ambapo Brazil waliibwaga timu ya Ufilipino katika nusu fainali goli 1-0.Magoli ya mechi zote yalifungwa kipindi cha pili huku Tanzania wakiumiliki mchezo kwa asilimia kubwa sana na watoto wa kitanzania walionyesha umahiri mkubwa sana mbele ya Balozi wa Tanzania nchini Urusi na pia maafisa wa Ubalozi walihudhuria kutazama mechi hiyo.
Kwa upande mwingine John Wroe ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa wa Shirika la Street Child United lililoshiriki kuandaa mashindano haya alimpokea balozi na ujumbe wake na kumpa zawadi na kisha baada ya mechi alimpa pongezi sana kwa ushindi uliopata Tanzania dhidi ya Uingereza.
Timu ya Tanzania imefika fainali tena ikiwa imeruhusu wavu wake kutikiswa mara moja tu chini ya mlinda mlango mahiri Sifaeli Geofrey na pia Tanzania inaelekea kutetea taji lake fainali kwani ndio mabingwa wa kombe hili tangu yalipofanyika mashindano haya mwaka 2014 nchini Brazil.
Post a Comment