TETESI ZA SOKA LEO MAY 15

 Mshambulizi wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang anasema alijiunga na klabu hiyo akiwa na imani kuwa Wenger atakabaki kama meneja kwa miaka kadhaa. (Evening Standard)
Mshambulizi wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang 

Mshambulizi wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang anasema alijiunga na klabu hiyo akiwa na imani kuwa Wenger atakabaki kama meneja kwa miaka kadhaa. (Evening Standard)

Steve Bould atachelewesha uamuzi ikiwa atabakia au la kama kaimu meneja wa Arsenal, anaposubiri kujua ni nani atakuwa meneja. (Telegraph).

Mambo muhimu yaliyotendeka siku ya mwisho Ligi Kuu England
West Ham walikutana na meneja wa Shakhtar Donetsk Paulo Fonseca saa chache baada ya mkataba wa meneja David Moyes kufika mwisho. (Mail)

Manchester City wanalenga kumsaini wing'a wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 25. (Star)

Ronaldo Jr atakuwa stadi wa kandanda kama babake?
Manchester United wanakumbwa na upinzani kutoka kwa Paris St-Geraon kumsania kiungo wa kati wa Shakhtar Donetsk Fred, 25. (Manchester Evening News)

Meneja wa Newcastle Rafael Benitez anasema hana nia ya kurejea Napoli kwa kuwa yuko kwenye mazungumzo na Magpie kuhusu mkataba mpya. (Calcio Napoli 24 - in Italian)

Benitez amefanya mazungumzo na kipa wa Paris St-Germain Alphonse Areola, 29. (France Football - via Metro)

Ronaldo alivyofunga bao la kushangaza dhidi ya Juventus
Real Madrid wako tayari kumwendea kipa Chelsea Thibaut Courtois, 26, wakati mbelgiji huyo akiingia miezi 12 ya mwiso ya mkataba wake.

Southampton wanataka kumsaini wing'a wa Celta Vigo Pione Sisto, 23. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark ana kipengee cha pauni milioni 36 cha kuondoka mapema kwenye mkataba wake.

Wing'a raia wa Morocco Sofiane Boufal, 24, amezungumzia nia yake ya kurejea ligi ya Ufaransa siku moja tu baada ya kukamilika kwa Premier League.(SFR Sport).

Kiungo wa kati wa Newcastle Jonjo Shelvey, 26, hatajumuishwa kwenye kikosi cha Uingereza kitakachoshiriki kombe la dunia kutokana rekodi yake mbaya kinidhamu. (Mirror)

Manchester United wako tayari kuilipa Napoli pauni milioni 44 kumpata beki Elseid Hysaj msimu huu. Raia huyo wa Albania wa umri wa miaka 24 atakuwa mlinzi namba saba ghalia zaidi duniani. (Sun)

Timu ya Tanzania street Academy yatinga fainaili
Everton watamfuta meneja Sam Allardyce saa 48 zinazokuja na wanakaraibia kumteua aliyekuwa meneja wa Watford Marco Silva. (Mirror).

Afisa mkuu mtendaji wa Arsenal Ivan Gazidis na mkrugeni mkuu Josh Kroenke wamemtambua kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal Mikel Arteta ambaye sasa ni kocha huko Manchester City kama mtu anayeweza kuchukua mahala pake Arsene Wenger kama meneja wa Arsenal. (Mail)

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post