chelsea ni moja ya club duniani zinazomilikiwa na mtu binafsi ambae ni Roman abramovich , lakini boss huyo anatambulika kwa kutoweza kumvulia kocha ikiwa timu inapata matokeo mabaya japo kwa msimu mmoja
Antonio conte anakuwa kocha wa 16 kuifundisha chelsea toka mwaka 2000 kwa wastani kila kocha amedumu kwenye club hiyo kwa mwaka mmoja na mwezi mmoja.
makocha mashughuli duniani wamepita kwenye club hiyo tangu mwaka 2000 mfano josë mourinho, fellipe scolari, claudio ranieri, Rafa benitez, Guus huddink, Andre villa boas, carlo anceloti, steve holland, ray wilkins , Roberto di mateo na wengine wengi.
Antonio conte mkataba wake unamalizika mwaka 2021 lakini sitarajii kuona akimaliza mkataba huo kwa muda husika bila kutupiwa vilago vyako.
unamkumbuka Roberto di mateo kocha pekee aliewapa taji la UEFA club hiyo kwa kupita katika migongo ya timu ngumu duniani akifanya come back ya historia pale darajani kwa kuwafunga napoli jumla ya goli 4-1baada ya kufungwa kwenye first leg na Napoli goli 3 -1.
Baadae alifanikiwa kumfunga barcelona na kucheza fainali na Bayern na kupata ubingwa ambao ni historia kwa club.
Lakini baada ya mwaka mmoja tu alitimuliwa kwenye club hiyo.
mpaka sasa sioni sababu ya kusema conte atabaki mpaka mwaka 2021 ikiwa timu inaenda kucheza UEROPA msimu ujao,
akitoka kuwa bingwa msimu uliopita , huku akipata matokeo mabaya kwenye mechi za hivi karibuni.
Sitashangaa kumuona manager mpya akiwa na chelsea msimu ujao kwa sababu tu namfahamu Roman abramovich.
Post a Comment