MATUKIO 6 YASIYOSAHAULIKA KUELEKEA KOMBE LA DUNIA 2018-RUSSIA

Kombe la dunia
Kombe la dunia ni moja ya tukio ambalo huwa linasubiri sana kwa hamu katika matukio yaliyopo duniani. Ni moja ya mashindano ambayo huwavutia hata wale ambao sio wapenzi wa mchezo huo murua wa mpira. Tukiwa tumebakiwa na siku 28 kuelekea kwenye mashindano kule Russia unaweza kuwa umeyaona matukio mengi sana katika world cup zilizopita lakini kama hufahamu hizi ndio historia tata na za kufurahisha katika mashindano haya.

 1.Kichwa cha zidane (2006) .

Hii ni moja ya kumbukumbu iliyoweka na nguli wa mchezo huu ambae ni kocha wa real madrid kwa sasa zinedine zidane baada ya kumpiga kichwa mchezaji wa italia marco materzazzi katika dakika ya 110 (extra time) baada ya kusemekana alimtolea maneno machafu kuhusu dada yake.

 2.Rene higuita alivyoiponza colombia .

Higuita ni moja ya makipa bora kuwahi kutokea kwenye mchezo wa soka na alifahamika kwa mbwembwe zake za kuokoa mipira golini kwake pia kuisaidia timu kwenye mashambulizi pale inapohitaji kushinda. ilikuwa kombe la dunia mwaka 1990 mechi dhidi ya cameroon kama kama kawaida yake alisogea mpaka katikati ya uwanja na akapewa basi na moja wa beki zake katika harakati za kutuliza mpira huo aliukosa na Rogger milla akauchukua mpira na kwenda kufunga na kuwapatia cameroon ushindi.

 3.Mkono wa mungu .

Hii ilikuwa kombe la dunia mwaka 1986 ambapo england walikutana na argentina katika hatua ya mtoano. Mnamo dakika ya 51 ya mchezo Maradona ambae alikuwa nyota wa argentina aliipatia argentina goli kupitia mkono ambapo kipa wa england peter shilton alipishana na mpira huo. Na mwenyewe maradona aliuita ni mkono wa mungu. lakini  cha kushangaza zaidi wachezaji 5 waliounda kikosi cha england walilipigia kura goli hilo na kuwa goli ya karne kupitia tovuti ya FIFA.COM . 

 4.AFRICA 

 Ni moja ya bara ambalo huwa linatoa vipaji vikubwa sana katika mchezo wa soka na kuvifanya vilabu vya ulaya kuwategemea sana mfano, george weah , didier drogba, Mo salah, Diouf, Rogger milla na wengine wengi ila Africa halijawahi kupeleka timu hata moja hatua ya nusu fainali toka mashindano haya yalipoanzishwa kwa mara ya kwanza. 

5.Kadi nyingi katika mchezo mmoja.

  Huu ni mchezo kati ya portugal dhidi ya Holland mwaka 2006 nchini ujerumani ambao ulikuwa ulichezeshwa na refarii valentin ivanov aliumaliza kwa jumla ya kadi 20 ikiwa nyekundu 4 na njano 16. 

 6. PELE 

 Huyu ndio baba wa mchezo huu kwa zile rekodi ambazo ameziweka na ngumu kuvunjwa akiwa amefunga zaidi ya magoli 1000 katika maisha yake ya soka. Ndie mchezaji aneshikiria rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kucheza katika fainali hizi akiwa na umri mdogo zaidi (17). 

katika fainali hizo kocha wa Brazil hakumuita pele katika chaguzi zake ila aliambiwa na rafiki zake pele kwamba kijana ni mchezaji mzuri na anaweza kuisaidia timu. Mechi yake ya kwanza alicheza dhidi ya sweden na katika mchezo huo alifunga hat -trick katika ushindi wa 5-2 na kuwa nyota wa mchezo na toka kumalizika kwa mechi alifunga karibia mechi zote alizocheza katika mashindano.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post