Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, ametoa siri ya Yanga kushindwa kupata alama tatu dhidi ya Rayon Sports katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. |
Yanga iliweza kulazimishwa suluhu ya 0-0 katika mchezo wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika ukiwa ni wa hatua ya makundi.
Kufuatia suluhu hiyo, Rage amesema kuwa aliwashauri Yanga mapema kufanya mazoezi ya saa 8 mchana huku akiwaomba wacheze dhidi ya Rayon muda huo watakaokuwa wanafanya mazoezi.
Rage ameeleza kama Yanga wangecheza majira ya saa nane mchana ingewapa ugumu wapinzani wao Rayon kutokana na utofauti wa hali ya hewa baina ya Kigali na Dar es Salaam.
Akizungumza na Radio EFM kupitia Sports Headquarters, Rage anaamini Yanga wangeweza kupata pointi tatu endapo wangecheza na wapinzani wao majira ya mchana tofauti na jioni wakati hali ya hewa ikiwa tulivu.
Yanga walikosa alama mbili jana na badala yake wakaambulia moja baada ya kushindwa kuifunga Rayon ya Rwanda.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au
kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Post a Comment