KIKOSI CHA UFARANSA KINACHOSHIRIKI KOMBE LA DUNIA

Paul Pogba

Mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial na Alexandre Lacazette wa Arsenal wameachwa nje ya kikosi cha Ufaransa kitakachoshiriki Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka huu.

Martial, 22, ameshinda mataji 18 na kuanza katika kikosi kilichoshinda kwa mabao 3-1 wakati wa mechi ya kirafiki na Urusi mwezi Machi.

Lacazette, 26, alishinda taji la mwisho kati ya 16 wakati wa mechi ya kirafiki na Ujerumani mwezi Novemba.

Kiungo wa kati wa Marseille Dimitri Payet hayuko kwenye kikosi hicho cha Ufaransa.

Beki wa Manchester City Benjamin Mendy ni kati ya wachezaji wa Premier League walijuuishwa licha ya kurejea uwanjani mwezi Aprili baada ya karibu miezi ishirini kufuatia jeraha.

Kiungo wa kati wa Chelsea N'Golo Kante na mshambulizi Olivier Giroud, kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba na kipa wa Tottenham Hugo Lloris ni wachezaji wengine wanaosakata kabumbu England waliojumuishwa katika kikosi hicho cha wachezaji 23.Anthony Martial na Alexandre Lacazette waachwa nje

Kiungo wa kati wa Stoke Steven N'Zonzi pia naye amejumuishwa.

Mshambuliaji wa Bayern Munich Kingsley Coman na kiungo wa kati wa Paris St-Germain Adrien Rabiot pia nao wameachwa nje.

Ufaransa wako kundi la C pamoja na Australia, Peru na Denmark.

Kikosi kamili cha Ufaransa:


Walinda Lango:

 Hugo Lloris (Tottenham Hotspur), Steve Mandanda (Marseille), Alphonse Areola (Paris Saint-Germain)


Walinzi: 

Lucas Hernandez (Atletico Madrid), Presnel Kimpembe (Paris Saint-Germain), Benjamin Mendy (Manchester City), Benjamin Pavard (Stuttgart), Adil Rami (Marseille), Djibril Sidibe (Monaco), Samuel Umtiti (Barcelona), Raphael Varane (Real Madrid)


Viungo wa kati: 

N'Golo Kante (Chelsea), Blaise Matuidi (Juventus), Steven N'Zonzi (Sevilla), Paul Pogba (Manchester United), Corentin Tolisso (Bayern Munich)


Washambuliaji: 

Ousmane Dembele (Barcelona), Nabil Fekir (Lyon), Olivier Giroud (Chelsea), Antoine Griezmann (Atletico Madrid), Thomas Lemar (Monaco), Kylian Mbappe (Paris Saint-Germain), Florian Thauvin (Marseille)

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post