TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO APRIL 09

Franck Ribery

Mshambuliaji wa timu ya Sheffield Wednesday- George Hirst mwenye umri wa miaka 19 - mwana wa mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo David - anatarajiwa kujiunga na Manchester United, huku klabu hiyo inayocheza ligi ya Championship ikitarajia kufaidi kutokana na hatua hiyo. (Mirror)

Viongozi wa Ligi ya Uholanzi PSV Eindhoven wanasema Everton wameonyesha nia ya kumtaka mkurugenzi wao wa soka Marcel Brands. (Sky Sports)

Mchezaji wa safu ya kati wa QPR Stephane Mbia, mwenye umri wa miaka 31, yuko tayari kuhamia klabu ya Atlanta inayocheza Ligi Kuu ya Marekani Kaskazini (MLS) kwa uhamisho wa bila malipo. (ESPN)

Kipa wa West Brom Ben Foster, 35, anataka kusalia katika klabu hiyo hata ikishushwa daraja kutoka Ligi ya Premia.

Kiungo wa kati wa Liverpool Mjerumani Emre Can, 24, ambaye mkataba wake wa sasa unafikia kikomo mwisho wa msimu huenda akaamua mustakabali wake katika kipindi cha wiki mbili zijazo, kwa mujibu wa mkuu wa Juventus Beppe Marotta. (Mediaset Premium)
Liverpool wameandaa mkataba wa miaka mitatu kwa ajili ya mchezaji wa safu ya kati wa Manchester United Mbelgiji Marouane Fellaini, huku Paris St-Germain na Monaco pia wakionyesha kumtaka kijana huyo mwenye umri wa miaka 30 ambaye mkataba wake katika Old Trafford unamalizika mwisho wa msimu. (L'Equipe -kwa Kifaransa)

Manchester United wana matumani ya kuwaadhibu zaidi mahasimu wao Manchester City kwa kusaini mkataba na Shakhtar Donetsk na mchezaji wa safu ya kati wa Brazil Fred, 25, mwisho wa msimu. (Mirror)

Mkuu wa zamani wa waamuzi England Keith Hackett haelewi ni kwa nini Martin Atkinson hakumfukuza wuanjani beki wa Manchester United Ashley Young wakati wa mechi yao dhidi ya Manchester City. Amesema vitendo vya Atkinson ni thibitisho tosha ya kuonesha ni kwa nini waamuzi wa England waliachwa nje ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu. (Telegraph)

Meneja wa Chelsea Antonio Conte anasema klabu hiyo haistahili kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya iwapo haiwezi kuzishinda timu kama vile West Ham. Hii ni baada ya klabu hiyo kutoka sare ya 1-1 na West Ham. (Times)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema pendekezo la Manchester City kwamba klabu hiyo inaweza kutumia uwanja wake wa mazoezi kwa maandalizi ya mechi ya marudiano ya robofainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumanne lilitolewa kwa kuchelewa.
Manchester United pia walikataa ombi kutoka kwa Liverpool wa kutumia uwanja wao wa timu ya wachezaji chipukizi. (Telegraph)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema huenda ndiye anayefaa kulaumiwa kwa klabu hiyo kulazwa na Liverpool na Manchester United. Hata hivyo amesema kutomakinika mbele ya lango kuna maana kwamba timu hiyo bado haijatosha kushindana katika ligi kuu bara Ulaya. (Times)

Everton inataka kutumia Euro milioni 25 majira ya joto yajayo kumnunua mchezaji wa West Ham Aaron Cresswell, mwenye umri wa miaka 28 ambaye pia ni beki wa kushoto katika timu ya England . (Sun)

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho anasema Pep Guardiola alidai Manchester City walipewa nafasi ya kumsajili Paul Pogba mwezi Januari kulipiza kisasi dhidi ya ajenti wake Mfaransa Mino Raiola. (Mirror)

Mourinho alionekana kugongwa na sarafu ya pauni iliyotupwa kutoka kwenye umati wa mashabiki wakati wa mechi ambayo Manchester United walishinda dhidi ya Manchester City Jumamosi, lakini Mreno huyo hakuripoti tukio hilo. (Star)

Bayern Munich watatoa fursa ya kusaini mkataba mpya kwa Mfaransa Franck Ribery, mwenye umri wa miaka 35, na Mholanzi Arjen Robben, mwenye umri wa miaka 34, ambao mikataba yao ya sasa inamalizika mwishoni mwa msimu huu. (Bild - kwa Kijerumani)

Mchezaji wa safu ya kati wa Tottenham Christian Eriksen anasema kumekuwa na malumbano ndani ya chumba cha kuvalia jezi za mpira juu ya ikiwa yeye ama Harry Kane ndiye anayefaa kutambuliwa kama mfungaji wa goli la pili la Spurs dhidi ya Stoke katika mechi ya Jumamosi ambayo walishinda 2-1. (Independent)
m, kupitia Express)

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post