TAARIFA KUTOKA YANGA KUHUSU KADI ZA OBREY CHIRWA


Mchezaji wa yanga Obrey Chirwa
Mabigwa watetezi wa ligi kuu Bara Young African "Yanga" imejibu tuhuma na imesisitiza kwamba, mshambuliaji wake Obrey Chirwa hana kadi tatu za njano na kufafanua kuwa mchezaji huyo ana kadi moja tu ya njano hivyo atakuwemo katika mechi dhidi ya Simba Jumapili wiki hii.

Wakati Simba ikitarajiwa kucheza na Yanga Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mechi ya Ligi Kuu Bara, taarifa ziliza­gaa kwamba Chirwa hatacheza sababu ana kadi tatu za njano.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh aliliam­bia Championi Juma­tano kuwa, Chirwa ana kadi moja ya njano aliyoipata dhidi ya Mbeya City wikiendi iliyopita, hivyo kocha anamuandaa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Simba.

“Chirwa hana kadi tatu za njano bali anayo kadi moja tu, si kama watu wanasema hivyo waache kusambaza uzushi, Chirwa atakuwa kikosini kama kawaida.

“Hata Ajibu (Ibrahim) naye amere­jea kiko­sini huyu alikuwa mgonjwa na wote wa­naendelea na mazoezi wapo fiti, la­kini kuhusu suala la kucheza ama kutocheza kocha ndiye atakayeamua,” alisema Hafidh ambaye ni miongoni mwa wanachama wanaohesh­imika sana miongoni mwa wanachama wa Yanga.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
WEKA EMAIL YAKO HAPA KUTUMIWA HABARI


Delivered by EDUSPORTSTZ

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post