MCHEZAJI BORA WA MWEZI MACHI LIGI KUU BARA



Mshambuliaji wa Lipuli ya Iringa, Adam Salamba amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Machi wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)Tanzania Bara.



Salamba alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Salum Kimenya wa Prisons na kipa wa Azam, Mwadini Ally katika uchambuzi uliofanywa wiki hii na Kamati ya Tuzo hizo.

Mshambuliaji huyo kwa Machi alionesha uwezo mkubwa na kuisaidia timu yake kupata mafanikio akifunga mabao matatu kwa dakika 270 alizocheza, ambapo Lipuli ilicheza michezo mitatu ikishinda miwili na kutoka sare mmoja na kupanda kwa nafasi moja kutoka ya nane hadi ya saba kwa mwezi huo.

Kwa upande wa Kimenya alicheza dakika 269 na kufunga mabao mawili, akiiwezesha Prisons kushinda michezo miwili kati ya mitatu iliyocheza na kutoka sare mmoja, ikipanda kutoka nafasi ya tano hadi ya nne.

Mwadini yeye alicheza dakika zote 270 ambazo timu yake ilicheza kwa mwezi Machi, ikishinda michezo yote mitatu iliyocheza, ikibaki katika nafasi yake ya tatu.

Kutokana na ushindi huo, Salamba atazawadiwa tuzo, kisimbusi cha Azam na fedha taslimu sh. Mil. Moja kutoka kwa wadhamini Vodacom.

Wachezaji wengine ambao tayari wameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi wa VPL msimu huu na miezi yao katika mabano ni mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi (Agosti), beki wa Singida United, Shafiq Batambuze (Septemba) na mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa (Oktoba).

Wengine ni kiungo wa Singida United, Mudathir Yahya (Novemba), mshambuliaji wa Mbao FC ya Mwanza, Habibu Kiyombo (Desemba), mshambuliaji wa Simba, John Bocco (Januari) na kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi (Februari).

Tuzo za Mchezo Bora wa jumla wa Ligi Kuu Tanzania Bara zinatarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu katika tarehe itakayotangazwa, ambapo licha ya Mchezaji Bora, pia kutakuwa na tuzo nyingine tofauti kwa kategori mbalimbali.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post