Daniel Amoah – Azam FC
KIVUMBI cha Ligi Kuu Bara kikiwa kimefikia patamu kipindi hiki cha lala salama ambapo Simba inaendelea kukimbiza kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo, kuna wachezaji wa kigeni kutok a nchi ya Ghana ambao w a m e e n d e l e a kuliteka soka la B o n g o n a k u o ng eza ushindani.
Kutokana na sheria na kanuni za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuruhusu uwepo wa wachezaji wasiozidi saba kwenye timu moja ya ligi kuu, imezifanya timu shiriki kufanya usajili wa wachezaji mbalimbali kutoka mataifa tofauti.
Championi Ijumaa limebaini kuwa, wimbi kubwa la wachezaji waliosajiliwa Bongo, Waghana ni wengi na wanafanya vizuri. Huu ni uchambuzi Waghana wanaofanya vizuri tangu kuanza kwa msimu wa 2017/18:
Enock Atta Agyei – Azam FC
Kiungo mshambuliaji, amejiunga na timu hiyo tangu msimu uliopita lakini ameanza kucheza msimu huu kutokana na awali kuwa na matatizo kwenye usajili wake.
Mghana huyo amekuwa akicheza kwa uhodari mkubwa kwenye nafasi yake jambo ambalo Azam wanajivunia kuwa naye kwani wakati anasajiliwa, alikuwa akipewa sifa nyingi kitu ambacho kweli amekuja kukidhihirisha ingawa timu yake hiyo imekuwa haina matokeo mazuri sana.
Daniel Amoah – Azam FC
Alisajiliwa msimu mmoja na Agyei, amekuwa katika kikosi cha kwanza tangu aliposajiliwa mpaka hivi karibuni alipopata majeraha makubwa ambayo anatarajiwa kukaa nje kwa takribani miezi tisa. Beki huyo mwenye uwezo wa kucheza kati na kulia, mkataba wake na Azam FC unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.
Yakub Mohamed – Azam FC
A n a u j e n g a vema ukuta wa Azam FC a k i s h i r i kiana na A g g r e y Morris. Yakubu alijiunga kikosini hapo misimu miwili iliyopita. Ubora wake unaweza kuwafanya mabosi wake kufikiria namna ya kumuongezea mkataba ili aendelee kusalia kikosini.
Bernard Arthur – Azam FC
A na c heza nafasi ya u s h a m b u l i a j i . A l i s a jiliwa kipind i cha usajili wa dirisha dogo msimu huu, akichukua nafasi ya Mghana mwenzake, Yahaya Mohammed. Wakati anasajiliwa mabosi wa timu hiyo walisema ni mshambuliaji hatari, lakini ameshindwa kuonyesha ubora wake wa kucheka na nyavu, amefunga bao moja pekee mpaka sasa.
Razack Abalora – Azam FC
Alisajiliwa baada ya kuondoka kwa Aishi Manula aliyetimik i a Simba mwanzoni mwa msimu huu. Kipa huyu ameziba vizuri pengo la Manula na amekuwa msaada mkubwa ndani ya kikosi hicho.
Nicolas Gyan – Simba
Ni winga ambaye kwa sasa anachezeshwa kama beki wa kulia na wakati huohuo winga. Wakati anasajiliwa mwanzoni mwa msimu huu, alitajwa kuwa ni mmoja wa washambuliaji hatari, lakini amekuja kubadilishiwa majukumu na sasa anachezeshwa nafasi tofauti na aliyokuwa akiicheza huko alipotoka.
Asante Kwasi – Simba
Ni msimu wake wa pili akishiriki Ligi Kuu Bara akiwa na timu tatu tofauti. Msimu uliopita alikuwa Mbao FC, msimu huu alianzia Lipuli FC kabla ya kuhamia Simba katika usajili wa dirisha dogo.
Licha ya kuwa beki wa kushoto pia amekuwa na uwezo mkubwa wa kufunga mabao ambapo katika orodha ya wafungaji kwenye Ligi Kuu Bara, ameweza kuwapiku washambuliaji kadhaa kwani mpaka sasa amefunga mabao nane.
James Kotei – Simba
Alijiunga msimu uliopita na kuisaidia Simba kuchukua ubingwa wa Kombe la FA. Msimu huu ameendelea kuwa mmoja wa wachezaji muhimu.
Licha ya kuwa ni kiungo mkabaji, lakini amekuwa akichezeshwa beki wa kati na amekuwa akifanya vizuri kitu ambacho kinawavutia mabosi wa benchi la ufundi la Simba lililopo chini ya Mfaransa, Pierre Lechantre.
Credit to globalpubrishers
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Post a Comment