Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia Chama Cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe |
Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia Chama Cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa yupo tayari kusema asante siku yake ya kutwaliwa ikifika kwani anauhakika amejitahidi sana katika kuuweka mkoa wake wa Kigoma kwenye ramani.
Zitto ameyasema hayo kupitia waraka wake ambapo amedai kwamba Kiongozi huwa anawaza kizazi kijacho na mwanasiasa huwaza uchaguzi ujao na kwa upande wake wakati anaingia bungeni alimuomba Mungu amsaidie kupitia yeye watu waone ufakhari kutoka Kigoma.
Aidha Zitto ameongeza kwamba hakuna mtu wa Kigoma anayeoona aibu kusema anatoka Kigoma hiyo ni kutokana na mshikamano walioutengeneza.
"Leo hata mola akisema Bwana Mwami funga siku zimetimia, nitasema Asante Mungu. Nitakuwa natabasamu maana nimeweka tofari zangu kupandisha nyumba yetu Kigoma juu ya msingi Imara kabisa. Watoto na Wajukuu watasema alikuwepo Mwami. Alikuwepo Kiongozi. Wataendeleza kazi" Zitto.
Ameongeza kwamba wanaowaza "Uchaguzi unaofuata hawana miadi na mungu. Wanaojiapiza kuhusu uchaguzi unaokuja hawajawahi hata kuchaguliwa kwenye kitongoji cha kwao walipozaliwa".
Mbali na hayo Mbunge huyo amefunguka kwamba demokrasia ndiyo imetoa nguvu kubwa ya kupiga hatua ikiwa ni pamoja na sauti ya kusikika "Anayetaka turudi kwenye ukiritimba ni adui mkubwa. Tutampiga tu".
Post a Comment