SAMATTA NA KICHUYA WALIBEBA TAIFA KISOKA




Timu ya taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya taifa ya DR Congo (The Leopards) kwenye mchezo wa kirafiki wa kalenda ya FIFA kwa mwezi Machi uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa taifa.

Mechi ilianza taratibu huku timu zote zikishambuliana kwa zamu hali iliyopelekea kipindi cha kwanza kumalizika bila timu hizo kufungana licha ya washambuliaji wa timu zote kufika langoni mara kadhaa.

Kipindi cha pili nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta aliwainua kwenye viti mamia ya mashabiki waliokuwa uwanjani dakika ya 74 baada ya kupachika bao kwa kichwa kufuatia kazi nzuri ya Ibrahim Ajib aliyeingia kipindi cha pili.


Baada ya bao hilo la kuongoza Taifa Stars waliendelea kushambulia na katika dakika ya 86 winga mshambuliaji Shiza Kichuya alipachika bao la pili kwa shuti kali alilolipiga akiwa nje ya eneo la 18 kufuatia makosa ya walinzi wa DR Congo.

Taifa Stars ilipoteza mchezo wake wa kwanza Machi 22 kwa mabao 4-1 dhidi ya Algeria ugenini hivyo leo imesawazisha makosa yake mbele ya DR Congo inayoshika nafasi ya 2 Africa ikiwa nafasi ya 39 duniani. Kwa viwango vya sasa Tanzania inashika nafasi ya 146.

Chanzo:eatv

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post